Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,345
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliasisiwa na kuanzishwa takribani miaka 22 iliyopita, hatua hii ilikuja kutokana na mageuzi makubwa yaliyokuwa yanashinikizwa na mataifa makubwa duniani na Umoja wa Mataifa.
Japo wahafidhina wa CCM pengine wasingependa kuona hili linatokea daima lakini kwa kipindi hicho hawakuwa na jinsi zaidi ya kuufyta mkia na kukubaliana na matakwa ya Magharibi na kwa mara ya kwanza Baba wa taifa aliifinyanga demokrasia kwa kukataa mapendekezo ya wengi kukataa mfumo wa vyama vingi wakipendekeza kuendelea na mfumo wa chama kimoja (lingekuwa suala la muda tu).
Nyerere aliendelea na msimamo wa kuruhusu demokrasia isiyokuwa na demokrasia kwani maana ya Demokrasia ni Udikteta wa maamuzi ya watu wengi dhidi ya maamuzi ya watu wachache.
Mwaka 1991 chini ya Mwenyekiti na mwasisi wa wazo la kuanzishwa chama hiki Edwini Mtei, CHADEMA ilianzishwa na makamu wake wa kwanza akawa Brown Ngululuki, Katibu Mwenezi wa kwanza akiwa Edward Balongo kutoka Kagera.
Mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) alikuwa mwanamama machachari bi Merry Kabigi kutoka Mbeya, ambaye pia historia inamtambulisha kama mbunge wa kwanza mwanamke wa Bunge la Jamhuri.
Aman Warid Kaburu baada ya kusafirishwa kwa juhudi za Mbowe na gharama zake kutoka New York Marekani hatimaye naye alikuja kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA na Katibu Mwenezi wa pili baada ya Balongo, kabla tamaa haijamzidi na kurudisha penzi kwa CCM.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani bwana Antony Nyaki huyu pia alifukuzwa kazi yake hiyo wakati huo kutokana na kumpokea nyumbani kwake Mtei wakati huo chama kikiwa katika juhudi za kumwomba Kaburu ajiunge nacho.
Bob Makani ambaye ni mwenyekiti wa pili wa chama hiki akifanya kazi nzuri katika kukiimarisha chama ngazi za mikoani, Mbowe akiwa mwenyekiti aliyempokea Makani kijiti pia wakati huo ndo alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa baraza la vijana, BAVICHA.
Huyu kamanda alikijenga chama from the grass root mpaka juu, tangu kinaanzishwa alikuwepo, sina haja ya kueleza mengi juu yake kwani kila mwana CHADEMA anautambua mchango wake.
Wapo pia makamanda walioshiriki katika harakati za kukiimarisha chama hiki katika hatua za mwanzo mpaka mwisho kama, Michael Shanga, Medadi Mutungi na Costa Shinyanga kutoka Kigoma na ikumbukwe kwamba kampeni za kwanza za vyama vya upinzani Tanzania ilizinduliwa Kigoma.
Chama kikaanzisha falisafa ya NGUVU YA UMMA "people'ss power" kikiamini umma kama sehemu ya serikali inayotoa ridhaa ya maamuzi na ruhusa ya mfumo wowote ule na huku itikadi yetu ikiwa ni mlengo wa kati unaoamini katika soko huria lenye kusimamiwa.
HISTORIA YA CHAMA NA VIONGOZI WAKE TANGU KIANZISHWE MPAKA SASA
Ikumbukwe kuwa chama kuanzia mwaka 1995 na 2000 hakikusimamisha mgombea yeyote wa nafasi ya urais kutokana na chama kuamini katika demokasia ya kusapoti vyama vyenye nguvu amabapo 1995 chama kiliazimia kumsapoti Mrema na 2000 Profesa Lipumba wa CUF lakini kiliweka wagombea katika nafasi zingine.
MAKAMANDA WALIOPOTEZEWA MAISHA NA POLISI KUTOKANA NA HARAKATI
5/1/2011, Polisi waliwafyatulia risasi na kuwaua wanachama 3 wa CHADEMA, polisi ikidai ilikuwa inazuia maandamano ya amani ya kupinga taratibu zilizomweka madarakani Meya wa Arusha Gaudenzi Lyimo, mpaka sasa hakuna aliewajibika.
27/8/2012, Polisi walimpiga risasi na kumwua Ally Shana Zone katika harakati za polisi kuzuia maandamano ya amani ya CDM M4C, hii ilikuwa ni Msamvu Morogoro.
2/9/2012, Polisi mkoani Iringa katika kijiji cha Nyololo mbele ya RPC wa mkoa Kamuhanda,walimpiga na kisha kumlipua kwa bomu mwandishi wa kujitegemea na aliekuwa anaripoti Chanell Ten TV Daudi Mwangosi, akafa akiwa kazini akitimiza wajibu wa taaluma yake.
21/7/2013, Polisi walifyatua bomu la mkono katika mkutano wa wazi wa mh mbunge John Mnyika baadae walidai lilifyatuka kwa bahati mbaya.
15/5/2013, bomu la mkono lilirushwa na kulipuka kisha kuwaua makamanda wa CDM huku watatu wengine wakijeruhiwa na risasi na bomu hii ilikuwa siku ya mwisho ya kuhitimisha kampeni za udiwani katika kata za Themi, Kaloleni, Elerai na Kimandolu mkutano ulikuwa ukifanyikia katika viwanja vya Soweto.
Imeandikwa na kamanda Nicholaus Kilunga wa Kibondo Kigoma, Tanzania!
nickkilunga@yahoo.com

- 1995 CHADEMA ilipata wabunge 4 na madiwani 42;
- 2000 CHADEMA ilipata wabunge 5 na Madiwani 75;
- 2005 CHADEMA ilipata wabunge 11 na madiwani 103;
- 2010 CHADEMA ilipata wabunge 49 na madiwani 467; hapo bila kuongeza chaguzi ndogo.