MAPENZI YA BANDIA.
Mara nyingi tumekuwa tukiskia neno bandia katika bidhaa,na vitu tofautitofauti,lakini katika mapenzi unaweza kuwa katika mahusiano yaliyotawaliwa na hisia bandia.
Ukipata mashine bandia kwa mfano ya kunyoa nywere kwa vyovyote ufanisi wako utakuwa mdogo sana katika namna ya kuonyoa na hata kasi yako,hivi ndivyo ilivyo pia katika mahusiano bandia.
Kwakuwa kupenda ni hisia omba sana usimpende mtu ambae anahisia za bandia dhidi yako,kwani atakufanyia vitu vingi sana kwa sababu anakuwa haoni shida si anahisia za bandia..
Katika hali ya kawaida tunagemea mme/mke aoneshe mapenzi ya dhati kila inapoitwa dakika,mtume paulo alishwahi kukaririwa akisema mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake mwenyewe.watu wengi sana huwa hawaelewi nini maana ya maneno haya.
Mwanamke mara zote anatakiwa kuwa mpole,mkarimu,mwenye hekima na uadilifu kwa mmewe/mchumba.
Hii haina maana mwanaume hatakiwi kuwa hivyo..laaa hasha mwanamke unauwezo mkubwa sana kumfanya mme wako atulie ndani ya nyumba au mahuusiano yenu kwa namna unavyoongea,na kuishi na mme/mchumba wako.
Wanawake wengi na hasa mabinti na vijna wakiume kiujumla wamekwa katika wakati mgumu sana kupata wenzi wema kwa sababu wengi hawana busara,uadilifu,hekima na upole...ndoa nyingi sana zimekuwa zikivunjika kwa sabab ya vitu vya hapo juu.
Na kwa kwa kuwa mwanaume ndio waliopewa jukum la kuanzisha mahusiano kulingana na jamii zetu basi wanawake wamekuwa hawakatai kila anamuomba mahusiano anakubaliana nae na hapa ndio chanzo cha matatizo yote..
Wanawake na wanaume wengi wameingia katika mahusiano kwa sababu za vitu vya kimwili,yaani fedha,chakula,mavazi nk na kwakuwa hivi vitu havina garantii basi vikiisha na mahsusiano pia yanaingia dosari...
Ulimi umekuwa ukichagiza sana katika kuharibu mahusiano kwani kuna watu hasa wanawake wepesi sana kutukana na huwa watu wa category hii hachagui mtu wa kumtupia tusi awe mama mkwe,au ndugu yyte ataporomosha tu.
Mathalani wewe ni mafanyakazi angaliavnyakati ambazo unagombana na mwenzi/mke wako...ukiwa na hela au ukiwa huna hela ukiona una mwanamke wa namna hio basi ujie huyo hakufai katka kuishi nae,yaani ana raha ya bandia,ukiwa nacho mtachek kikiisha atanuna.kama umemuoa basi vumilia lakini kama hujaingia kwenye ndoa nae basi ukisoma makala hii chukuwa hatua tafta mwanamke/mwanaume atakae kujali hata ukiwa mkiwa.