Hisa za NMB

Danny Massawe

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
1,299
Reaction score
765
Wana jf nawasalimu nyote na kuwatakia a good weekend...nilikuwa naomba ufafanuzi kidogo kwa wenye kujua mambo ya hisa za NMB. Nilinunua hisa za NMB wakati nikiwa mwanafunzi mwaka 2007 zilikuwa 100@600 jumla nilitoa elfu 60. sasa nataka kujua hizi hisa samani yake imefikia sh. ngapi kwa moja?.pili na je hisa zitakuwa zimeongezeka idadi?..tatu nataka kujua kwa nini gawio/devidend huwa dogo sana ninapocheki kwenye akaunt yangu huw linakuja lakini huwa halifiki hata elfu kumi. kwa wanao fahamu naomba wanijuze maana naona kama hakuna significant faida ninayopata kutokana na hizi hisa za NMB.
 

Ninachofaham mimi ni kuwa bei ya hisa za NMB kwa sasa ipo juu sana zaidi ya Tsh 2000/= kufaham zaidi tembelea website ya DSE huwa wanatoa thamani za hisa.
 
hisa moja kwa had jana ni tsh 2690 mara hisa 100 ni tsh 269000 ukitoa elf 60 unapata tsh 209000 kama faida kama ukiziuza leo hizo hisa. ila kama huna haraka nazo ziache hadi ukistaaf ukaziuze utapata hela nzuri tu si chini ya milion 10.
 
dividend mara nyingi ni asilimia 10 had 12 ya hisa zako kwa bei ya sasa (current market price). mfano 10% ya 269000 ni tsh 26900. kama ni chini ya hapo mtembelee wakala aliyekuuzia hisa akueleze kwa nini dividend ni ndogo. labda wanajisahau au kukosea kupiga hesab. Pia uwe unaingia website ya soko la hisa (dse) kujua maendeleo ya hisa zako
 
hadi jana ilikuwa 4960, hisa mia ukiuza utapata 496000, ulinunua chache ila si mbaya, kuhusu dividend huwa had watangaze inawez kuwa mara moja au mbil kwa mwaka, na dividend huwa inalipwa per share. Mfano kama walitangaza 70 per share manake utachukua 100* 70 ambayo ni 7000 itategemea wametangaza kiasi gan kw share, Returns ya uwekezaji wa hisa ipo sehem mbili kwanza ni capital gain (ongezeko la thaman ya hisa) na pili ni dividend
 
jamani nawashukuru sana kwa elimu mliyonipa itanisaidia sana... pia nitatembelea DSE kujua zaidi.....ila mimi nilinunua benki sasa sijajua idadi ya hisa huwa inaongezeka au ni thamani ndio inaongezeka peke yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…