Hisa za DSE

Majige

Member
Nov 11, 2006
33
56
Soko la hisa wanauza wanauza hisa kama kampuni. Wadau je kuna matumaini zitalipa hasa kipindi hiki ambapo bei za hisa kwa kampuni nyingi zinaporomoka?
 
Hisa zikienda chini, ndio wakati wa kununua na zikienda juu uza. Unataka kununua wakati bei iko chini na kuuza wakati bei ziko juu ili upate faida kubwa. Kwa hivyo, huu ndio wakati wako wa kununua kwa sababu ziko chini. Lakini, fanya research ya kutosha kabla huja nunua hisa za kampuni yeyote. Angalia kama wana management nzuri, ubora wa bidhaa zao na kama wanauza kwa wingi, na angalia future investments...n.k
Nategemea watalaam wa mambo ya hisa watachangia zaidi.
 
The best time to buy a stock is when then "price is low" and best time to sell a stock is "almost never". Theory ya biashara yyt ni kubuy at low price and to sell at high price, lakini inashauriwa u invest in long term (growth investment) yani ununue hisa leo ambazo miaka 20 badae zitakufanya uwe tajiri mkubwa. Ila ukifanya speculation wataalam wanasema ni ngum kuotea lini soko linapanda na lini litashuka coz unaweza ukabuy leo afu soko likashuka zaidi au ukasell leo soko likapanda zaidi. Chamsingi kujua ni what is the real value ya hy kampuni compared to bei ya hisa zake coz yaezekana bei ya hisa iko juu saaana kulinganisha na thamani halisi ya kampuni. Mambo mengine ni management, strong product na R&D. But unaweza soma vitabu vya watu kama Benjamin Graham, philip Fisher na Warren Buffet wameelezea vzr hili swala.
 
Mawazo yangu;

1. Hisa za DSE sio nzuri sana za kununua na kuuza kama wachangiaji wanavyosema hapo juu. Hizi hisa ni kama zipo stagnant, inachukua muda mrefu sana bei kubadilika. Nashauri ni bora ununue ili uje kupata dividend na sio kuuza na kununua.

2. Ukitaka kununua na kuuza hisa kama biashara tafuta masoko yaliyochangamka kama JSE au NYSE. Kwasababu huko bei inabadilika over night. Na pia uwe na mtaji mkubwa ili uweze kununua na kuuza hisa nyingi ili upate faida.
 
Haya masoko mengine ni ya nchi gani? Duh umeniogopesha mkuu maana nina wazo la kuanza kuwekeza kwenye hili soko baada ya kuckia faida zake

Nimesema hapo, hayo ni mawazo yangu baada ya kufanya utafiti wangu.

Na wewe fanya utafiti wako.
 
Inawezekana kununua hisa kwenye masoko ya nje ya nchi na tahadhari gani zinapaswa kuchukuliwa. Mwenye info sahihi plse afunguke hapa.
 
Inawezekana kununua hisa kwenye masoko ya nje ya nchi na tahadhari gani zinapaswa kuchukuliwa. Mwenye info sahihi plse afunguke hapa.
Hivi capital account kwenye balance of payments ya tz imerekebishwa ??nakumbuka IPO ya safaricom Kenya wabongo tulishindwa kununua.
 
Back
Top Bottom