General Agents
Member
- Oct 7, 2015
- 93
- 60
Lengo la uzi huu ni kutoa mawazo yangu binafsi nionavyo kuhusu hisa za CRDB.
Ongezeko la watoa huduma za kifedha hapa nchini sio habari nzuri sana kwa wanahisa wa CRDB. Sasa hivi Bank za jumuiya kama Njombe, Mbinga, KCBL zimekuwa zikifanya vizuri na kuongeza idadi ya wateja. Pia SACCOS nyingi zmeongeza wanachama na zmekuwa kimbilio la kutoa mikopo nafuu kwa wanachama wake.
Biashara kubwa ya Bank ni kukopesha, lakini Bank zetu zmekuwa zikitegemea zaidi kununua treasury bills ambazo kwa sasa itakuwa changamoto kwao kwa kuwa serikali imeagiza pesa zake zote kwenye hizi Bank za kibiashara kuwekwa BoT. Hili agizo litalifanya bank za kibiashara haswa CRDB ambao walikuwa wanafanya juu chini wawe na accounts na mashirika au taasisi za serikali kutetereka kiutendaji ukizingatia hili agizo limekuja ghafla na hawakulitegemea kabisa.
Ni dhahiri mwaka huu faida ya CRDB itapungua kwa kiasi kikubwa na itawawia vigumu kutoa gawio kwa wanahisa wake kwa mwaka wa fedha wa 2016, ambao utafanyika 2017. Hii itapelekea wanahisa wengi kutaka kuuza hisa zao kwa ghalfa hali ambayo itapelekea kuwa na hisa nyingi zinazouzwa sokoni na kusababisha kuporomoka kwa bei.
Mara nyingi management ya Bank huwa inapenda kuwatia moyo wanahisa wake kuwa mambo yanaenda vizuri, kama alivyofanya Kimei juzi. Management hufanya hivyo makusudi ili kuhakikisha wanahisa hawauzi hisa zao. Kwa mfano Management ya Supermarkets za Uchumi ilikuwa ikiwatia moyo wanahisa wake hivi hivi na kuwa peti peti kwa kuwapa expectations kubwa, kilichotekea ni super markets za Uchumi kuangukia pua na kufunga branch zake Tanzania na Uganda. Hii ilisababisha Management kupelekwa mahakamani na wanahisa.
Soko la hisa ni soko lililojaa siri sana, sio huru kama wengi tunavyodhani. Kwa Tanzania bado hili soko ni changa sana, kwa mwananchi wa kawaida ni bora ukawekeza katika biashara nyingine. Kama unabisha waulize wanahisa wa Precision wamefaidika vipi na hisa zao.