Hili wazo la Wakenya la kuanzisha Mamlaka ya Kudhibiti Dini, Watanzania tunalionaje, tuige?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,111
Nakumbuka mzee Lowassa kwenye Uchaguzi mkuu wa 2015 alisema endapo atachaguliwa ataanzisha Wizara ya Dini

Sasa kupitia Citizen TV baadhi ya Wabunge wa Kenya wametaka ianzishwe Regulatory Authority kwa mambo ya Dini na wametaka Mapadre, Mashehe, Wachungaji, Maaskofu na Viongozi wote wa Dini Wachunguzwe mali walizonazo na namna walivyozipata

Hii ni kufuatia kuuawa kwa Watu wengi ambao wamekutwa na alama za kufungwa waya na kubondwa na Vitu vizito vichwani na kisha kila familia kuzikwa kwenye kaburi moja.

Inadaiwa Mackenzie ambaye ni mchungaji alikuwa anatoa mafundisho potofu na kutumia nguvu za giza

Mwenzako akinyolewa wewe zako tia maji, Je Tanzania nasi tuanzishe Mamlaka ya Kudhibiti Dini kufuatia utitiri wa Huduma za Kiroho

Alhamis Barikiwa sana!
 
Dini yoyote ya "serikali " au "usalama" ni yao na si ya Mwenyezi Mungu.
In most cases they are cults, just another opium for the masses.

Hao Wakenya watafute chanzo halisi cha tatizo sio kuja na blanket "solutions " ambazo huongeza tatizo au kuhamishia kusikopasa.
 
Mwanzo iliripotiwa waliokufa Kwa kutokula muda mrefu,

BAADAYE inagundulika waliuwawa na baadhi Wana makovu.

Nafurahi kusikia yule Nabii feki wa Mombasasa Eze naye amekamatwa baada ya police kuripoti mara kadhaa watu kufia ktk compas zake.

Nashauri sirikali isiingie Kanisani, iishie nje. MANABII wawe na viongozi na wawadhibiti manabii wa uongo.

Zumaridi kuendelea kuachiwa aendelee na USHETANI wake, atapiga tukio na tutatizamana kama hatukuwa kukimwona. MANABII feki wanajulikana, wapotezwe,


Security zajua nini kinaendelea. Wawatumie watumishi wa Kweli KUWAPOTEZEA wa uongo, warudi viringeni kupiga uganga.

Maombi yafanyike sehemu za wazi, Si vyumbani au ktk makazi ya watumishi Kwa Siri.
 
Niliwahi kuandika hapa Uzi kuhusiana na hilo kelele zimekua nyingi ila ni muhimu kwakweli.
 
Tangu Pastor Mashimo aitolee njaa zake YOUNG-AFRICAS.
Hizi dini naziona kama mchezo wa siasa tu!

Hivyo tuombe uzima Mungu akijalia niwe namimi hata Mchungaji wa mbuzi pale mwananyamala-komakoma :(
 
Tatizo ni kwamba serikali nazo ni mfumo mfumo wa huyo huyo muasisi wa Dini,yaani Lucifer,so nani amfunge paka kengele sioni.Itakuwa danganya Toto tu.Ni swala la panya kuuma na kupuliza.
 
Waige tu Kagame kila shehe au padre au mchungaji awe na cheti cha degrii kinachotambulukana na mamlaka ya serikali period!
 
Yaani ije wizara au mamlaka ya kudhibiti dini lakini iwe ni dini za kikristo. Uislamu hauna makando kando ya kudhibitiwa.
 
Back
Top Bottom