Hili swali huwa linaninyima raha ugenini

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,116
8,652
Kwa nini mnaua ma albino!? Ndilo swali linaloniuma sana kila nikiulizwa, nilikumbana nalo juzi wakati Taifa Star inaifunga Botswana nikiwa naelezea umahiri wa mchezaji Samatta ukiachilia mbali daraja la Kigamboni ambalo humvutia sana mwenyeji wangu hasa ukiliangalia kwa video za usiku. Leo tena ukurasa wa gazeti la Soweto wamelipa kipaumbele
f32423a2cb76b2faeefe7bfbee7d6075.jpg
 
Mkuu samahani sana hebu ongezea na hili..Kwanini mnaua vikongwe kwa imani za kishirikina tuu? Kikongwe kikishakua na macho mekundu ujue watakihusisha na ushirikina!!
 
Mbona jibu rahisi mkuu!
Au huwa unaliogopa jibu kulitoa mbele ya mwenyeji wako huko?
We mwambie tu ukweli huku Tz ya watu walio gizani wanaamini watu hawa ni dili.
 
Tupo nyuma ya wakati mno, tuna evolve kwa speed ndogo.

Wazungu huu ushirikina wa kutoa kafara za watu waliufanya miaka elfu nne iliyopita wakati kina Abraham anataka kuua mwanaye.

Hadi mwaka 1300 wazungu walikuwa wana amini mwanamke mwenye pua ndefu ni mchawi.

Baada ya black death walipata akili wakajua haya mambo ya kiimani na ushirikina ni upotofu mtupu.

Ndipo wakaingia kwenye scientific era, exploration, industrial revolution, enlightenment na sasa wapo hapo walipo.

Maisha ya waafrika yamekuwa sugarcoated na westerners, lakini kiuhalisia tupo nyuma mno.
 
Kikubwa mi nadhani ni njia za mafanikio ya waliofanikiwa kutokuwa wazi, leo ukimuuliza aliyefanikiwa amepitia njia zipi, hawatoi majibu yenye mashiko.

Njia kama ufisadi, ujambazi, uuzaji wa madawa nk haziweki wazi ktk jamii. Kuzificha na watu kukosa haya majibu, wanakimbilia kusadiki njia hizi za kishirikina. Na hata hao wanaotajirika, kwa njia hizi hupenda kujificha ktk kivuli cha ushirikina kwa usalama wao.
 
Mkuu samahani sana hebu ongezea na hili..Kwanini mnaua vikongwe kwa imani za kishirikina tuu? Kikongwe kikishakua na macho mekundu ujue watakihusisha na ushirikina!!
Kaka nishawahi kuleta uzi miaka kadhaa nyuma Kuhusu hizi imani. Moja na hii tabia ziko sana kanda ya ziwa japo karibu Tanzania nzima hivi vitendo vimeshamiri sana. Sababu kuu ninazozifahamu mimi ni life style ya kabila langu la kisukuma. Ukifuatilia kwa ndani kabisa ikiwezekana ufanye safari utagundua hata hapo zamani ili uwe Mtemi ilikupasa uwe na sifa za ziada (mtaalamu wa elimu ya gizani), uchimbaji madini kuhusishwa na uwepo wa nguvu za ziada, kuwepo kwa waganga wengi karibia kila ukoo, na elimu pia. Kukosekana kwa elimu ya kutosha ilisababisha kila mtu akiugua au kufa basi hawakuamini kama ni maradhi tu yamesababisha mwisho ni kabila letu na makabila yaliyo na uhusiano na wasukuma kuchukua eneo kubwa Sana Tanzania.
 
Kikubwa mi nadhani ni njia za mafanikio ya waliofanikiwa kutokuwa wazi, leo ukimuuliza aliyefanikiwa amepitia njia zipi, hawatoi majibu yenye mashiko.

Njia kama ufisadi, ujambazi, uuzaji wa madawa nk haziweki wazi ktk jamii. Kuzificha na watu kukosa haya majibu, wanakimbilia kusadiki njia hizi za kishirikina. Na hata hao wanaotajirika, kwa njia hizi hupenda kujificha ktk kivuli cha ushirikina kwa usalama wao.
Kuna ukweli kabisa hapa. Hongera
 
Back
Top Bottom