Hili ndio kosa pekee alilokosea Hayati Magufuli

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,583
15,351
Ukiwa unasafiri hujui unakokwenda na muda utakaotumia kufika utachoka mapema sana.

Katika mikakati yote hakutupa timing ya lini tutafika anapotaka ili walimu waanze kuajiliwa kama zamani, mishahara iongezeke, watu wapande madaraja, gharama za bidhaa zirudi kama ilivyokuwa kabla.

Alibadili gia ghafla na mambo yote ghafla ili baadae mambo yarudi katika ubora wake badala yake kila siku bora jana. Hadi anaondoka nilikuwa sioni ni lini tutaanz Kula matunda ya mikakati yake.

Kosa hili tume ya uchaguzi iliangalie ilani iwe na mipango inayotekelezeka kwa miaka ambayo mgombea atakuwa madarakani kikatiba. Mgombea au chama asiache viporo ili kwenye kampeni asiombe aongezewe Muda ili amalizie.

Miradi inayovuka miaka mitano ihamishiwe kwenye dira za kitaifa.

Alamsiki.

Tunamkumbuka kwa mazuri, kwa mabaya hatulaumu bali tunajifunza (lessons Learned)
 
Hilo wala sio kosa lake kubwa, Viongozi wengi duniani wana kuwa na priorities zinazoweza kutofautiana na stakeholders wengine katika nchi

Kosa kubwa la Hayati ni kutokubali kushaurika / kushauriwa
 
Mimi ninacho amini ni kitu kimoja tu! Kama Taifa, tumejifunza mengi kupitia yeye! Na hivyo hatutokuja kurudia tena makosa siku za usoni.

Mzee alikua anaelekea kutugeuza kuwa mazombi! Mpaka sasa hata siamini kama tumenusurika.
 
Ukiwa unasafiri hujui unakokwenda na muda utakaotumia kufika utachoka mapema sana.

Katika mikakati yote hakutupa timing ya lini tutafika anapotaka ili walimu waanze kuajiliwa kama zamani, mishahara iongezeke, watu wapande madaraja, gharama za bidhaa zirudi kama ilivyokuwa kabla.

Alibadili gia ghafla na mambo yote ghafla ili baadae mambo yarudi katika ubora wake badala yake kila siku bora jana. Hadi anaondoka nilikuwa sioni ni lini tutaanz Kula matunda ya mikakati yake.

Kosa hili tume ya uchaguzi iliangalie ilani iwe na mipango inayotekelezeka kwa miaka ambayo mgombea atakuwa madarakani kikatiba. Mgombea au chama asiache viporo ili kwenye kampeni asiombe aongezewe Muda ili amalizie.

Miradi inayovuka miaka mitano ihamishiwe kwenye dira za kitaifa.

Alamsiki.

Tunamkumbuka kwa mazuri, kwa mabaya hatulaumu bali tunajifunza (lessons Learned)
Ndio maana ilikuwa lazima tumlazimishe aongeze muda, ile ilani ilikuwa na kurasa nyingi Polepole alisema ilivunja rekodi na bado yalichomekewa na maono yake wakati wa kampeni.
 
Back
Top Bottom