Hili nalo ni kwa faida ya uislamu!?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,794
287,947
Waislamu wapinga upimaji ukimwi kabla ya ndoa

Shabani Matutu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

UKIMWI ni miongoni mwa maradhi yanayowasumbua wataalamu duniani kote, unawaumiza vichwa kutokana na kutokuwa na tiba hadi sasa.

Licha ya ukweli kwamba baadhi ya mataifa makubwa, waganga wake wametangaza kupata dawa za kutibu ugonjwa huo, lakini kitaalamu bado haijathibitika kuwepo kwa dawa hiyo.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani (WHO), limetangaza kuwa Bara la Afrika, linaongoza kwa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi, ambapo Afrika Kusini ina idadi kubwa zaidi.

Ukiachilia takwimu hizo, hivi karibuni Waislamu kutoka Afrika Kusini, wametoa msimamo wao na kuushangaza ulimwengu baada ya kutangaza kuandaa maandamano ya kupinga sheria ya wananchi wa nchi hiyo kupima kabla ya kufunga ndoa.

Pamoja na kwamba wanaharakati mbalimbali wa ukimwi duniani wapo mstari wa mbele kuwataka wanandoa kuhakikisha wamepima kabla ya kufunga ndoa ili kupunguza kasi ya maambukizi.

Jumuiya au taasisi zinazojishughulisha na ukimwi zinaamini kwamba iwapo watu walio katika uhusiano wataoana bila kupima, kutakuwa na uwezekano wa kuambukizana iwapo mmoja kati yao ameambukizwa.

Na pia iwapo wataoana upo uwezekano wa kuzaa mtoto ambaye atakuwa wamemuambukiza ugonjwa na hatimaye kuisababishia dunia kuwa na kizazi kilichoambukizwa maradhi ya ukiwmi.

Waislamu wa nchi hiyo wamekuwa wakipinga kitendo hicho wakikitafsiri kama moja ya ubaguzi kwa wanadamu. Na kwenda mbali zaidi kudai kuwa kitendo hicho kinawabagua wale wenye ugonjwa huo kutopata ruhusa ya kuoa, kwa kuwa atakuwa amenyimwa haki yake ya msingi ya kuoa.

Hata pamoja na jumuiya hizo kutoa elimu kuhusu maambukizi kwa jamii lakini Waislamu nchini Afrika Kusini wameonekana kwenda kinyume na maazimio ya Shirika la Afya Duniani (WHO), kuhakikisha wanakamilisha lengo lao la mwaka 2025 kutokomeza maambukizi ya ukimwi duniani.

Baada ya Waislamu wa nchini humo kutangaza pingamizi hilo wamejikuta wakipata pingamizi kutoka kwa wanaharakati wa masuala ya ukimwi wa nchini humo, ambao wametupilia mbali wito huo.

Mashirika ya nchini humo yamedai kwamba kwa wito huo, Waislamu watakuwa wanarudisha nyuma mapambano dhidi ya ukimwi na badala yake watakuwa wanahamasisha ongezeko la maambukizi.

Wanaharakati hao walikwenda mbali zaidi kwa kuwashutumu Waislamu hao na kudai kwamba hatua hiyo inakwenda kinyume cha katiba ya nchi yao.

Mmoja wa wanaharakati maarufu wa ukimwi wa nchini humo, Fatima Ahmed, amepinga kauli hiyo na kudai kwamba inaharibu afya za wanajamii na itaendelea kuleta ubaguzi dhidi ya watu.

Kabla ya Waislamu kutangaza hatua yao ya kutaka kuandamana kupinga wanandoa kutopima kabla ya kufunga ndoa, lilitolewa na mbunge wa upinzani wa nchi hiyo, Maulana Rafeek Shah.

Shah, aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kwamba kitu kinachotakiwa kufanywa na Serikali ya Afrika Kusini si kuwapinga Waislamu, bali ni kuielimisha jamii ya Kiislamu kuhusu vitisho vya ugonjwa huo.

Alisema iwapo jamii ya Kiislamu itafahamishwa kuhusu hatari ya ugonjwa huo, wataelewa na kuwa tayari katika kusaidia mapambano ya ukimwi.

Wakati hayo yakitokea nchini Afrika Kusini, kwa jirani zetu Kenya, utafiti wa hivi karibuni kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi, unaonyesha kuwa maambukizi yameongezeka, kwani takwimu zinaonyesha zaidi ya watu 1,400,000 wameambukizwa.

Utafiti huo umefanywa na Shirika la Kupambana na Ukimwi na Magonjwa ya Zinaa (NASCOP), pia shirika hilo limedai kwamba idadi ya watu waliojitokeza kupima imeongezeka maradufu.

Shirika hilo limedai kwamba serikali nchini Kenya imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa raia wake ili wafikie malengo ya kutokomeza au kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Serikali za Afrika zimekuwa katika mstari wa mbele kutangaza athari za ukimwi na jinsi ya kujikwamua na ugonjwa huo kwa raia wake, lakini cha kushangaza, mpaka leo takwimu zinaonyesha kuwa Afrika inaendelea kushika kasi kila kukicha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom