Hili nalo neno......

sakapal

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
1,804
Reaction score
1,425
Kwenu wanaume na wanawake wa jukwaa hili,

Hili jambo huniwazisha sana. Ni kawaida kabisa pale ambapo mwanaume anapotoka nje ya ndoa basi watu wote wanawake kwa wanaume watamlaumu mke wake kuwa ni chanzo. Hali hii imezoeleka hadi kupelekea wanawake kukaa kimya na kutosema hata kwa wachungaji wao pale waume zao wanapotoka nje ya ndoa hata kama kwa kurudi rudia kuogopa kualaumiwa. Pia hali hii imewafanya wanawake wengi kuishi kwa woga kwenye ndoa zao maana jamii na wanaume wamehalalisha kuwa kama mke hamfurahishi mumewe katika kila nyanja basi mumewe atatoka nje. Mabinti wanafundishwa mumeo mfanyie hili na lile na usipofanya atatafuta nje. Yaani mkazo na msukumo hauwi ili wote mfurahie ndoa bali ili mwanaume asitoke nje.
Na mwanaume akitoka nje utasikia mke wangu hanifanyii hili na lile na kila mtu anakubali kweeeli hapo hukuwa na jinsi. Bado najiuliza kwa upande wa pili mbona hali ni tofauti? Sijawahi ona watu hakusema kuwa mwanamke anapotoka nje ni sababu ya mume wake, hata kama mumewe anamfanyia kila aina ya manyanyasho ataambiwa avumilie, najiuliza uvumilivu ni kwa wanawake tu au na wanaume Pia?
Ukiangalia kiapo cha ndoa kila mmoja anaapa kuwa mwaminifu kwa mwenzie katika hali zote, shida na raha, ila mwanaume katika shida tena ndogo sana anakimbilia kutafuta faraja nje ila mwanamke yeye anatakiwa kuvumilia. Najiuliza, hivi wanaume wao hawapaswi kushika kiapo cha ndoa? Maana hali hii imewafanya Pia wanaume wengi kuwachukulia wake zao for granted yani mradi amemuoa basi kazi yake imeisha, hashughuliki kumfurahisha na kumfanya ajisikie wa thamani maana anajua hata asipofanya hivyo mkewe lazima atamfanyia mema kwa kuogopa mume atatoka nje. Wakati mwingine wanandoa wanapokosa mtoto mume atatafuta nje watu wanamulewa kuwa hakuwa na jinsi ila mke akifanya hivyo atapewa majina yote mabaya.
Tutafakari kwa pamoja, upo na mwenzi wako ili usitoke nje au upo naye sababu unampenda na utafanya kila uwezalo kumfurahisha?
Mwanaume utakuta anasema mke wangu mkorofi, mke wangu mkali, mke wangu hajui kupika, mke wangu hili na lile Ndio maana anatoka nje ila pale anapogundulika na mke anataka kuondoka anasema uliapa kukaa nami katika shida na raha, swali mbona wanaume hamkai na wake zenu katika shida???

Nimejikuta najiuliza hili swali, wewe mdada, mwanamke, mkaka, mwanaume hasa mlio kwenye mahusiano ya muda mrefu mnalionaje hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…