Hili la posho za vikao Serikali imekua double standard

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,851
5,620
Heshima kwenu wanajanvi. Wote mtakumbuka posho kwenye sekta zote za umma zimeondolewa.
Pamoja na kwamba imeongeza ukali wa maisha kwa wafanyakazi walio wengi wote nikiwa miongoni tumeipongeza serikali. Kwani watu walitumia kama njia ya kufanya ubadhirifu na imesaidia kubana matumizi ya serikali.
Swali ni kwamba kwanini hili haligusi wanasiasa? Hapa namaanisha Bunge.
Ina maana hawa ni binadamu tofauti?
Kwanini wabunge hasa wa CCM washangilie posho za vikao kufutwa kwenye taasisi za umma na wakalie kimya posho za kukaa bungeni.
Kwanini serikali ifute posho za vikao vyote kwenye taasisi za umma.. Na wabunge wanao pokea mshahara, daily subsistance allowance na marupurupu mengine, walipwe sitting allowance iliyo futwa kwingine. Je serikali inawahonga wabunge?je hii sio double standard?

Karibu tujadili
 
Hivi unajua wale ni binadamu...wana matamanio....wana uhitaji wa hela...kibaya zaidi hawana ule ubinadamu wa kumtetea wa chini...wakisikia sheria inahusu kumnyanyasa mfanyakazi wa chini wanapiga makofi meza hadi meza inatoa machozi...ila wajue suala linawahusu wao..weeeee
 
Na kwahili swala la kusitisha promotion za wafanyakazi limekaaje? Juzi niliona hii thread lakini imefutwa kwanini?
 
Hii ni double standard ya Magufuli. Kuna mbunge mmoja anaitwa Fenera au Fenela wa cdm alisema kupitia itv analipwa sh milioni 4.3 ukitoa allowances mbalimbali. Magufuli amefuta posho za vikao katika taasisi mbalimbali za umma, iweje wabunge wanaojinasibu kutetea wananchi wao walipwe posho. Na wabunge wao wameshindwa kutoa tamko la kumuunga mkono rais kukataa posho. Hii inadhihirisha kuwa wapo kimaslahi zaidi
 
Double stands sio double standard, yote ya yote mtoa mada tambua kwamba mkuki kwa kitimoto kwa binadamu mchungu. UKITAKA MOTO UWAKE NCHI HII WAWAFITIE WABUNGE POSHO YA Makalio
 
Double stands sio double standard, yote ya yote mtoa mada tambua kwamba mkuki kwa kitimoto kwa binadamu mchungu. UKITAKA MOTO UWAKE NCHI HII WAWAFITIE WABUNGE POSHO YA Makalio
Asante kwa kusahisha ingawa nafikiri hauko sahihi. Double standard =is the application of different sets of principles for similar situations
 
Inauma sana, hawa Wabunge ifike muda waondolewe hizi posho na baadhi ya malipo yasiyo na ulazima ili tupate Wabunge wenye moyo wa kweli wa kuwakilisha wananchi. Wengi wao wanaingia bungeni kwa njia za rushwa wakitegemea kurudisha hela zao kwa njia hizi. Ikitokea malipo yanakuwa sawa na watumishi wengine, tutapata wawakilishi makini wasiopenda rushwa na ushirikina.
 
Mi nawaambia. Ikitokea posho na malipo ya wabunge na mawaziri yakapunguzwa, watu watalazimishwa kugombea ubunge. Hapo ndipo tutapata wabunge wazalendo sio kama hawa wapiga vijembe na wagonga meza
 
Back
Top Bottom