Mlalamikaji daily
JF-Expert Member
- May 19, 2014
- 736
- 1,613
Mheshimiwa Rais nikupongeze kwa kasi yako unayoendelea nayo.Naandika hili nikiwa na uhakika kuwa utalipata.
Ni kweli wakuu wa shule wamepewa jukumu la kuongoza shule na wanatakiwa kuwajibika kwa nafasi zao kama wakuu.
Mheshimiwa Rais, kauli yako kuwa shule ikiwa na division zero(0)
nyingi basi walimu wakuu wawajibike, napingana nayo kwa sababu zifuatazo:
1.Walimu wakuu sio wasababishi wa watoto kufeli.Hebu fikiri mheshimiwa raisi shule ina walimu watatu,haina vitabu,haina madawati,je hao watoto watafaulu vipi?
2.Hali ya walimu.
Je walimu wametengenezewa mazingira gani ya kusababisha wafundishe kwa ufanisi? Mishahara midogo,watu wana madai,hakuna nyumba n.k Je wanafunzi watafaulu vipi?
Katika matokeo ya kidato cha nne tumejionea shule 50 bora zote ni za binafsi.Ina maana tatizo lililosababisha shule za serikali kufanya vibaya ni wakuu wa shule?
3. Mheshimiwa suala hilo pia litasababisha udanganyifu katika mitihani maana wakuu wa shule watafanya mbinu zao wanazojua ili wafaulishe wakuridhishe wewe ilihali katika uhalisia wanafuzi hawakufaulu.
Asante kwa kusoma waraka wangu.
Mwananchi.