Hili hapa shairi la wajumbe

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
1,526
2,000
Wajumbe

Simu walinipigia,
Sifa zangu kunipatia,
Wakanisihi nitie nia,
Wajumbe sio watu wazuri

Walisema nakubalika,
Nitapita bila shaka,
Kura zao watanipa uhakika,
Wajumbe sio watu wazuri

Mara nyingi tulikutana,
Mipango tuliweka bayana,
Nilipambana usiku na mchana,
Wajumbe sio watu wazuri,

Ukimbini tulipoingia,
Sera nikawamwagia,
Kwa kweli walishangilia,
Wajumbe sio watu wazuri,

Kura zikawekwa mezani,
Kila mtu na yake mkononi,
Wamenitenda wajumbe wala siamini,
Wajumbe sio watu wazuri

Sikupata hata kura moja,
Hata ya wale tuliokuwa pamoja,
Wajumbe wamenifanya kihoja,
Wajumbe sio watu Wazuri
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,409
2,000
Wajumbe

Simu walinipigia,
Sifa zangu kunipatia,
Wakanisihi nitie nia,
Wajumbe sio watu wazuri...
Ndo ukome kuweka nia,
Na kushindwa kujipigania,
Wajumbe nawapa mia,
Wewe kinda kutumbukia..😂

Wajumbe wajumbeni,wamekutenda ujumbeni
Kikao walikuwekea,kikaango kukupatia
Kwa joto lililomea,ukaiva na kutokomea😜

Yajayo yanafurahisha,umebaki kuosha sufuria
Wajumbe wamekacha,umebaki na wako msufuria..😜
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom