Hija ya vipapa Tunduru

Joined
Jan 7, 2014
Posts
13
Reaction score
1
Vipapa au watoto wamisionari wa kanisa katoliki Tanzania waliutikisa mji wa Tunduru kwa maandamano ya aina yake. Waliwasili Tunduru 12/6/2014 na kuweka kambi katika seminari ndogo ya Muhuwesi. Juni 15 waliingia katika mji wa Tunduru kwa chereko.

Wakiwa Muhuwesi walipata semina mbalimbali km watoto na athari za vyombo vya habari, watoto na Imani, watoto na maisha ya watakatifu nk.

Pia walifanya mashindano ya kusoma Biblia kwa kichwa. Kana kwamba haitoshi kulikuwa na mashindano ya ngoma za utamaduni kutoka mikoa mbalimbali. Mji wa Tunduru ulitikiswa kwa ujio wa watoto hao zaidi ya 3,000.

Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu (Pontifical Mission society for Holy Childhood) lilianzishwa na Askofu Charles Auguste de Forbin Jansen 1785 huko Ufaransa.

Askofu Charles alianzisha kikundi cha watoto ili kuwasaidia wapagani wamfahamu Yesu Kristo. Kongamano la kitaifa hufanyika kila baada ya miaka mitatu. Lilifanyika Iringa, likaenda Zanzibar, kisha Mahenge na mwaka huu Tunduru.
 

Attachments

  • CIMG1593.JPG
    52.8 KB · Views: 142
  • CIMG1618.JPG
    48.4 KB · Views: 129
  • CIMG1628.JPG
    60.3 KB · Views: 109
  • CIMG1632.JPG
    56.1 KB · Views: 143

samahani kama nitakukwaza ila kwanini hukuipeleka jukwaa la dini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…