Wala JK hana kosa ktk hili. Rais kwanza anastahili kupongezwa kwa kujali jinsia ktk uteuzi, labda huyu mama kama aliwasilisha vyeti feki hili ni suala jingine na vyombo vya sheria vipo nadhani vinaweza kufanya kazi yake.
Kuhusu uwindaji bila kibali, hili ni kosa kwanza la wale waliokamatwa kwa sababu wewe unajua kwamba ili uwinde ktk game reserves lazima upate kibali. Kwa hiyo ilikuwa ni jukumu la waliotumwa kuomba kibali maliasili na utalii, lakini kama walikurupuka tu eti kwa sababu walitumwa na DC, wao ndo wajinga na wananstahili adhabu kali.
Hii ndo inayotufanya watanzania wakati mwingine tumlaumu rais kikwete lakini ukichunguza unakuta watendaji ndo wazembe na wengi wao ni vihiyo. Unapotumwa na mkuu wako wa kazi kitu fulani, siyo kwamba kakwambia usifuate sheria wakati unatekeleza majukumu yako yanayohusu kile ulichotumwa, labda awe amekupa barua kwamba fanya na usifuate sheria.
Tukio hili ndo linaonyesha kansa ya utawala wa CCM kwamba ukitumwa na boss basi usifuate sheria. Kumbuka yule mkurugenzi wa halimashauri fulani alikataa kulipia malazi ya ugeni wa makamuwa rais dk shein wilayani kwake kwa sababu sheria haimruhusu kufanya hivyo kwani msafara wa shein unalipiwa na serikali kuu, lakini DC wake asiye jua sheria alisha mshikia bango DED kuwa kafanya makosa.
Kwa hiyo kwa tukio hili watendaji wote wa umma lazima mjifunze kufuata sheria pale unapotumwa kufanya chochote na mtu yeyote hata kama ni rais, labda tu kama amekupa maandishi yanayosema usifutae sheria.