Hii picha imebeba siri kubwa

Mkuu tutajie hizo siri. Mi naona wala sio siri, kila kitu kiko wazi-Mmeipenda wenyewe ndi ndi ndi, Chaguo Lenu wenyewe ndi ndi ndi............................
 
Jamaa amepigika na "sababu" iko mbele yake. Tumaini limepotea kwa hiyo anaendelea kuangalia picha isiyoweza kumpa msaada. Usije shangaa baadaye ukipita mtaa huo utakuta sehemu muhimu ya picha hiyo haipo.
 
Ha ha ha!!
mkuu si kila maskini kasababishiwa umaskini na viongozi wengine ni wao wenyewe mtu anapata kazi nzuri lkn pesa anatumia kwa pupa badala aanze na A anaanza na Z hatari sana..!!
 
Yawezekana ndivyo watu walikuwa wakiangalia picha ya Mandela SA wakidhani akitoka jela na kuwa rais, basi waafrika wote watakuwa mamilionea na kuwa na hali bora kama au zaidi ya wazungu. Mpaka anatutoka waliomfata wamezidi kuwakandamiza hao hao waliowaweka madarakani. Rangi zile zile na moto ile ile.
 
Huyo jamaa anajuta sana sana
atakua anaimba ule wimbo wa "If I could turn back the time"
 
"Sikutegemea kama goli la mkono linaweza kuleta maajabu ya namna hii!" Mawazo ya mzee akiangalia matokeo ya goli la mkono...
 
jamaa bado hajawahi kuamini kama kweli BWANA YULE ndiye wa sasa maana alijua maisha bora na million 50 za kijiji zipo kweli.


swissme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…