hii ni sawa kweli?

Graca

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2011
Posts
471
Reaction score
152
wadau hebu nisaidieni hili maana nimenishangaza sana leo na hata sijui nyie mtalichukuliaje hususani wanandoa.

ni hivi nilikua na friend wangu tunapata soga mbili tatu muda uende kila mtu ajisogeze kwake. kama mjuavyo kuna watu hususani wanaume wanapenda kuweka simu mezani. bahati simu yake ikaita na kwa vile nilikua karibu nikaona picha ya mrembo amepiga kimini kwenye display kabla hajapokea simu, akaongea nae then nikamtania nani huyo? akanijibu ah huyu ni mpenzi wangu.. kwakua mkewe namjua nikamdadisi kidogo nae akafunguka akaniambia ni nyumba ndogo yake na ana mpango wa kumfanya mke maana anampenda sana. sikutaka kumhoji sana nikapotezea.

sasa nikabaki na maswali mengi sana kichwani hivi:

ina maana ni anampenda sana huyo binti mpaka afikie hatua hiyo?
je simu ikiita mkewe aione itakuwaje?
huo ujasiri mpaka wa kuweka hiyo picha kwenye namba ya huyo bidada kaupata wapi ilihali ana mke tena wa ndoa?
sasa kama hana mapenzi kwa mkewe si bora amuache kuliko kumuumiza hivi?

wanajf nyie mnalionaje hili maana mh nnapata woga kabisa wa kuolewa
 
Hao ndo wanaume!!!!!!!!!
Evelyn Salt hebu waite waje watuelezee kwann hii hali.. kweli usimwonee huruma mkeo? hatukatai kweli wengine wanakua na nyumba ndogo lakini si inakuwa siri? naona kama yy amejiachia sana
 
Last edited by a moderator:
Yani mapenzi ya siku hizi ni kama maigizo. Itakuwa labda mkewe hana tabia ya kuchunguza simu ya mumewe au mume amemkataza asiguze simu yake hata ikiita.
 
Yani mapenzi ya siku hizi ni kama maigizo. Itakuwa labda mkewe hana tabia ya kuchunguza simu ya mumewe au mume amemkataza asiguze simu yake hata ikiita.

Miss Mwakipunda je ikitokea imeeita na mkewe yupo karibu na akaiona je? ni kwamba hajali maumivu atakayopata..

aagh inasikitisha sana jamani.
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
he he..chezeya wanaume!!

BelindaJacob, mh ni kazi..hata kama ndoa ni ndoana but hii imepitiliza. ina maana anaishi nae kwa mazoea tu wala hajali tena hisia za mkewe na yupo tayari kwa lolote au ndo yale mambo ya akufukuzae hakwambii toka?
 
Last edited by a moderator:
Huyo ni mlafi tu....kuna wengine hawana hata sense ya guiltiness.
 
Usiogope kuolewa dada, wanaume wenye mapenzi ya kweli, wasio na tamaa na wanaoheshimu ndoa zao bado wapo. Muombe mungu akuongoze umpate mume bora na si bora mume.
 
Mi hata sishangai kitu ka hicho coz hata huku nliko, mwenyewe haogopi hata kupigiwa ucku wa manane na anaanza kuongea kimahaBa yani hata Mungu hawamwogopi wanasahau walimuahidi Mungu wataishi na wenza wao kwa shida na raha na hawatashughulika na wengine


Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii forum
 
Hii sio sawa has kimaadili, hatuwezi kumukumu yeye au wanaume wote kisa ushamba wa huyu jamaa....
 
halafu mkiambiwa kagueni simu za wapenzi wenu mnagoma.........


Ila si unajua wanaume ni mabingwa wa kutafuta viranga nje na kuharibu ndoa zao? Usishangae....... Tena ukichunguza utakuta kaanza na mkewe akiwa na suruali mosha mashati mawili na godoro....akishapata dudu inalia mbwata mbwata anamwona mkewe hafai.....
 

mamiiiiiiiiii mbona umenisusa sana mwenzio?? nimekukosea nini mpendwa wangu binti yangu wa rohoni.
 
Usiogope kuolewa dada, wanaume wenye mapenzi ya kweli, wasio na tamaa na wanaoheshimu ndoa zao bado wapo. Muombe mungu akuongoze umpate mume bora na si bora mume.

grand-mal na mapresha niliyonayo moyo wangu utatoboka kwa kweli.. labda tu nipatr mume mwenye hofu ya Mungu.
 
Last edited by a moderator:

Eversmilin Gal pole mwaya maana najua inauma kuwa na mtu ambaye hajali hisia zako wala maumivu.. aah bora niendekeze ubachela tu maana naona hawa watu wengi wao tabia zao zafanana.
 
Last edited by a moderator:
Hii sio sawa has kimaadili, hatuwezi kumukumu yeye au wanaume wote kisa ushamba wa huyu jamaa....

kabanga nashukuru sana..so ww unaona ni ushamba tu wa jamaa?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…