Sio sawa sana, anachopaswa ni yeye kutathmini ugonjwa wako, matokeo ya maabara, hali yako kiafya, matatizo mengine uliyonayo na kadhalika halafu ajue ni dawa gani nzuri kwako. Baada ya hapo atakuambia nakuandikia dawa fulani, ndipo wewe useme kama unaafiki. Tusitumie dawa kwa mazoea jamani, bali ni kwa hali halisi ya ugonjwa na mgonjwa.