Hii ni sahihi kweli?

king_azy

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2014
Posts
265
Reaction score
965
Najua kila mtu anakumbwa na mitihani ya kipato, lakini kumuachia mkeo aanze kuomba msaada kwao ni sahihi kweli? Mimi kama hali haiko shwari nitapambana kama nikishindwa hata nitakopa mimi kama mimi lakini siwez kuruhusu mke wangu aombe ndugu zake labda kama naumwa sijitambui

Lakini kuna wanawake wameolewa lakini kila kunapokuwa na shida ndogo wanaomba kwao na saa zingine mume anatoa simu yake ili mke apige kwao.Msaada inarususiwa lakini pale inapobidi ila ndugu yako kukupigia simu eti anaomba hela hata ya panadol na mwanaume yupo mzima wa afya kweli? Na unakututa si mara moja imekuwa ni kawaida.

Hivi ni sahihi au mimi ndo nina shida ya kuelewa dunia?
 
Hivi ni sahihi au mimi ndo nina shida ya kuelewa dunia?
Hauna shida yoyote, ukiona mtu anafikia hatua hiyo basi majukumu yake yanamshinda...msaada ni sawa kuomba lakini kwa kitu kigumu Sana Ila siyo Panadol duh😲
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…