hakuna cha waangalizi wala nini ccm imeshinda kihalali bila ubishi
CCM kwa ulevi tu wa madaraka inafanya hujuma ikiamini haitangoka madarakani.Lakini siasa za wakati huu ni za vijana. Na vijana hawawataki hata kuwasikia.Nawatahadharisha msijidanganye katu.Mtangolewa tena vibaya maana mtakuwa ni maadui badala ya wananchi wenzao vijana hao.Kwa nini hamuoni? Mna macho lakini hamuoni?Mna masikio lakini hamsikii? Hali ya upepo ni mbaya mno kwenu CCM."Mwalimu aliwahi kusema siku wananchi watakapo amka wakakuta mmewaibia mali zao, viongozi wote wa ccm mtaishia jela."Kama hamjaishia jela lakini wananchi hawa wameanza kuamka. Umma the sleeping giant is awekening, take care.Ushauri wa bure.
1)Msifanye uonevu, hasa kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kuwanyanyas wapinzani na wananchi wanaotaka mabadiliko kwa ujumla.
2)Anzeni kujitayarisha kupokea nafasi ya upinzani kama wenzenu, KANU, UNIP, MMD kwa kuwa hiyo ndiyo nafasi yenu mliyo nayo kiuhalisia kulingana na hali ilivyo.
3)Mikakati yenu ya ushindi inazidi kuwapalia makaa ya moto iacheni kwa sababu siyo sustainable.
4)Acheni siasa za chuki kuwenu kama baba ambaye anakosolewa na wanae.Ktk kipindi cha miaka 50 lazimz mmefanya makosa mengi na mengine kama kuhujumu uchumi kwa makusudi, yako dhahiri.
5)Undeni tume huru ya uchaguzi, tume huru itawaondoa ktk mtego mliojinasisha wenyewe,kama mna akili mnaelewa ninachokisema.
6)Tafakarini yaliyowapata kina Mubarak,Gadaffi, Laurent Gbago n.k.Linganisheni nani mwenye akili kati ya hao niliowataja hapo na na Banda wa Zambia.
7) Vijana wa kizazi hiki ni moto ulao mtaliwa. Tafakari.Propoganda haisaidii maana wana mawasiliano supa.
8)Fanyeni utafiti kwa nini vyombo kama Intelligence services na security agencies hazikuwazuia vijana kuwaondoa kina Mubarak, Ghadafi nk.
9)Kwa herini tuonane 2015.