Hii ni hatari kwa Tanzania miaka ijayo

chief1

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,415
1,409
Kumekuwa na utitiri wa vyama mbalimbali vya kikanda na kikabila katika maeneo mbalimbali katika nchi yetu, vyuoni kuna vyama vya wasukuma, wahehe, wachagga nk, hata mitaani kuna viumoja flani vya makabila au watu kutoka mkoa flani au wilaya flani..vyama hivi vinaanzishwa kwa lengo kuu kusaidiana wakati wa shida?

Swali: je watanzania tumeiacha ile jadi yetu ya kusaidia na kupendana kama ndugu kwa ujumla wetu?

Jibu ni hasha! kwa hivyo kwa moyo mmoja nasema hivi vyama ni haramu!!

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, namnukuu "Mnadhani ni muhimu sana kujana makabila yenu?umuhimu wa makabila umebaki kwenye matambiko tu na si vinginevyo"
Binafsi nikiwa chuoni nilikataa kabisa kujiunga na chama cha wasukuma, atakayekusaidia wa kwanza ni Jirani yako na siyo kabila lako,
Hili ni jambo la kuepukwa kama ukoma!!
Msituletee mambo kama yaliyotokea Rwanda 1994.
Waziri wa elimu na Mh Rais kemea hili.

Hata humu JF kuna watu waanzisha vi thread eti watu wa mkoa flani tukutane hapa
Mkutane kufanya nini kama sio ukabila huo..
 
Mleta Mada Una Ugonjwa Hatari Sana Unaoitwa HOFU-High Opacity Fear Of Unkown. Yani Kuna Blanket Zito Sana La Fikra Kandamizi Linaloiseta Akili Yako.
 
Naona mleta mada amejaribu kuonyesha uelewa wake.Atakuja pia siku kusema makabila yafutwe yasitajwetajwe jambo ambalo ni hatari.Haiwezekani mtu wa kigoma mfano akafia Dar ukadhani utaenda kuomba serikali imsafirishe huyo mtu au mtoa mada ukiambiwa uchangie matatizo yakila aliyepo mkoa mwingine akitaka kurudi kwao wewe upo tayari?Kama huelewani na ushirika naona ungeomba ushauri kwanza
 
Mleta Mada Una Ugonjwa Hatari Sana Unaoitwa HOFU-High Opacity Fear Of Unkown. Yani Kuna Blanket Zito Sana La Fikra Kandamizi Linaloiseta Akili Yako.
Mleta Mada Una Ugonjwa Hatari Sana Unaoitwa HOFU-High Opacity Fear Of Unkown. Yani Kuna Blanket Zito Sana La Fikra Kandamizi Linaloiseta Akili Yako.
hivi inakuwaje mtu unasubiri mwenzio alete mada ili tu umkashifu badala ya kuchangia alichokisema?hata kama hukubaliani nae tafuta njia mbadala ya kumjibu.
 
Ukifanikisha la makabila, utazame pia hili la ongezeko la dini mitaani!
 
Kumekuwa na utitiri wa vyama mbalimbali vya kikanda na kikabila katika maeneo mbalimbali katika nchi yetu, vyuoni kuna vyama vya wasukuma, wahehe, wachagga nk, hata mitaani kuna viumoja flani vya makabila au watu kutoka mkoa flani au wilaya flani..vyama hivi vinaanzishwa kwa lengo kuu kusaidiana wakati wa shida? Swali: je watanzania tumeiacha ile jadi yetu ya kusaidia na kupendana kama ndugu kwa ujumla wetu? Jibu ni HASHA, kwa hivyo kwa moyo mmoja nasema hivi vyama ni haramu!!
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, namnukuu "Mnadhani ni muhimu sana kujana makabila yenu?umuhimu wa makabila umebaki kwenye matambiko tu na si vinginevyo"
Binafsi nikiwa chuoni nilikataa kabisa kujiunga na chama cha wasukuma, atakayekusaidia wa kwanza ni Jirani yako na siyo kabila lako,
Hili ni jambo la kuepukwa kama ukoma!!
Msituletee mambo kama yaliyotokea Rwanda 1994.
Waziri wa elimu na Mh Rais kemea hili
Hata humu JF kuna watu waanzisha vi thread eti watu wa mkoa flani tukutane hapa
Mkutane kufanya nini kama sio ukabila huo..
I think Magu ataaddress hii tabia inayoota mizizi kila siku
 
mbona hii ina miaka ukienda kivule matembele kun wakurya tu, kimara temboni wachaga, bunju chalinze wazaramo, asidi aachi asili.
 
kama wanaungana kwa kutaka kusaidiana tu na sio kufarakanisha makabila ya wenzao sioni tatizo. watanzania tunavumiliana sana makabila tofauti maana tumeoleana sana.mke wangu ni kabila tofauti na langu na kila mmoja anahudhuria vikao vya kabila lake bila mfarakano wowote.
 
hivi inakuwaje mtu unasubiri mwenzio alete mada ili tu umkashifu badala ya kuchangia alichokisema?hata kama hukubaliani nae tafuta njia mbadala ya kumjibu.
Ukiona hivyo ujue ni mmoja wa viongozi wa vyama hivyo anayetafuna michango ya wanachama. Wengi wameibiwa katika vyama hivi.
=============
Binafsi napenda ushirikiano usiojari ukabila, dini, na mambo mengine wakati wa shida na raha.
 
Mleta mada we uko wapi na unazunguzia watz wa wapi Wa mtwara, musoma
UK , marekani,china kote huko watz wanaumoja wao sijakuelewa
 
Kumekuwa na utitiri wa vyama mbalimbali vya kikanda na kikabila katika maeneo mbalimbali katika nchi yetu, vyuoni kuna vyama vya wasukuma, wahehe, wachagga nk, hata mitaani kuna viumoja flani vya makabila au watu kutoka mkoa flani au wilaya flani..vyama hivi vinaanzishwa kwa lengo kuu kusaidiana wakati wa shida? Swali: je watanzania tumeiacha ile jadi yetu ya kusaidia na kupendana kama ndugu kwa ujumla wetu? Jibu ni HASHA, kwa hivyo kwa moyo mmoja nasema hivi vyama ni haramu!!
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, namnukuu "Mnadhani ni muhimu sana kujana makabila yenu?umuhimu wa makabila umebaki kwenye matambiko tu na si vinginevyo"
Binafsi nikiwa chuoni nilikataa kabisa kujiunga na chama cha wasukuma, atakayekusaidia wa kwanza ni Jirani yako na siyo kabila lako,
Hili ni jambo la kuepukwa kama ukoma!!
Msituletee mambo kama yaliyotokea Rwanda 1994.
Waziri wa elimu na Mh Rais kemea hili
Hata humu JF kuna watu waanzisha vi thread eti watu wa mkoa flani tukutane hapa
Mkutane kufanya nini kama sio ukabila huo..
Nakuunga mkono mtoa mada, kma watu wanataka kutengeneza chama, basi kisihusishe kabila moja hko chama kiwe mchanganyiko hata kwa kujumuisha marafiki wa makabila tofaut tofaut na sio hzo habar za kabila moja ndo mwanzo wa ubaguzi unapoanzia.. madhara ya hivyo vyama hatuta yaona leo miaka michache hpo badae ndo mtayaona.. mtoa mada umeona mbali..
 
Siku ukienda kuishi UK, marekani ,China au kwingineko na ukakuta watz wenzio wanachama fulan utakikataa na kujiunga na cha wakenya au wanigeria ? Na je ukijiunga na chama cha watz wenzio ina maana huipendi Africa au ? Au inamanisha kusambaratika kwa bara la Africa ? Think big kijana
 
binafsi naona hivi vyama vina saidia, mfano kuna moja wetu wa Rombo hapa Dar na mikoa mingine, umoja huu unasaidia kama mtu akipata msiba, anasaidiwa kusafirisha kwenda nyumbani(Rombo) kuzika, na mipango mingine ya mazishi,
au labda kuna kijana au rafiki yako katoka Rombo kuanza maisha au shule mjini na hana pa kushukia ili ajipange kwanza,
au kuna kijana wako unamfahamu hana ajira ila unataka umdhamini kwenye biashara au ajira ila peke yako huwezi kuna Warombo wenzako watakusaidia kumdhamini au kumpa hata ajira na kumkopesha mtaji kwa kuwa unaifahamu familia yake na unafahamu anapokaa kule nyumbani (Rombo)

lakini hii haimaanishi kuwa hatuchangamani au hatusaidii watu wa mkoa mwingine, mtu yoyote tu ili mradi unajua unaweza kumuamini
 
Back
Top Bottom