kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,086
JANA katika mfululizo wa makala haya yanayoangalia mambo ‘muhimu unayopaswa kuyajua kuhusu kuhamia Dodoma’, tuliangalia hasara ambayo inaweza kuwakumba wanaonunua viwanja mjini humo kwa wenyeji.
Kwa kifupi nilisema ardhi yote ya manispaa iko chini ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), hivyo yeyote anayetaka kununua ardhi aende kwenye mamlaka hiyo na kujua taratibu za kununua kiwanja na utaratibu wa kujenga. Leo ninaangalia kitu kingine ambacho nimeona ni muhimu kwako kukijua kwani baada ya kufika mjini Dodoma; mji ambao ndiyo makao makuu ya serikali, kila ninachokiona, najaribu kukilinganisha na mji mkuu wa biashara wa Dar es Salaam. Miongoni mwa maeneo ambayo nayaangalia ni pamoja na usafiri wa umma.
Nashuhudia magari aina ya Hiace maarufu kama ‘vipanya’ yakiendelea na kusafirisha abiria mjini Dodoma. Nakwenda hadi kwenye vituo ambavyo magari haya hupakia na kushusha abiria. Nakuta magari mengi yakiwa yakipakia abiria kwa mtindo wa kupanga foleni. Vipo vituo viwili vya daladala. Kimoja kinajulikana kama kituo cha Stendi Kuu kutokana na kuwa jirani na kituo cha mabasi yaendayo mikoani. Kingine ni cha Jamatini. Jina limetokana na msikiti mkongwe wa Jamatini uliopo eneo hilo.
Unapotaka kutoka mjini Dodoma kwenda maeneo ya Kikuyu, Area D, Mnadani, Msalato, Nkuhungu, St Gema, kituo sahihi cha kwenda ni cha Jamatini. Daladala zinazokwenda Nanenane, Nzuguni, Kisasa, Swaswa na kupita vituo mbalimbali ikiwemo CBE, zinapatikana kituo cha Stendi Kuu. Ikiachwa vituo hivyo vikuu, naendelea kufuatilia vya njiani. Miongoni mwa ninachobaini, ni nidhamu ya madereva na makondakta ya kushusha abiria kwenye vituo vilivyopangwa.
Msamiati wa ‘msaada’ kutoka kwa abiria naona hauna nafasi kubwa hapa Dodoma. “Abiria wanafahamu kwamba lazima ashuke kwenye vituo vilivyopangwa,” kondakta mmoja wa daladala ananieleza kuwa wanaogopa kushusha holela kwani trafiki wakiwakamata, wanaadhibiwa ipasavyo. Wakati nikiendelea kufuatilia usafiri huu wa umma, nakumbuka suala zima la wapiga debe na namna ambavyo kwa namna moja au nyingine wamekuwa kero kubwa si tu kwa abiria, bali hata wenye magari katika jiji la Dar es Salaam.
Nakumbuka namna ambavyo imefikia hatua, wapiga debe wamehodhi vituo vyote vya daladala huku wakitoza ‘ ushuru’ kila chombo cha moto kinachosimama kituoni kupakia abiria. “Lazima utoe hela ya ‘kitengo’ (wapiga debe) usipotoa unajitakia madhara,” mmoja wa madereva wa bajaji wanaopakia abiria Ubungo kwenda Tandika, jijini Dar es Salaam anasema. Wakati nikiendelea kuwaza adha hiyo ya wapiga debe na namna mamlaka za jiji la Dar es Salaam zimekuwa zikijinasibu kuwakomesha, mjini Dodoma naona hali ni tofauti.
Ninachobaini ni kwamba, ingawa wapigadebe wapo kwenye vituo hivyo vikubwa vya kupakia abiria, kwa upande wa vituo vya njiani, hawapo. Nikiacha suala la wapiga debe, nabaini kwenye daladala hawakosekani waliosimama kama ilivyo kwa Dar es Salaam. Hata hivyo, magari ya Hiace (vipanya) badala ya Coaster, yanawapa wakati mgumu abiria ambao ni warefu kwa kuwa hulazimika kujipinda. Njia chache, hususani ya kutoka Jamatini kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ndiyo naona magari aina ya Coaster.
Hata hivyo, faida waliyo nayo watumiaji wa usafiri wa umma wa Dodoma, ni kwamba, hata kama atasimama kwenye daladala, hakawii kufika kwa kuwa hakuna msongamano wa magari barabarani kama ilivyo Dar es Salaam. Mambo mengine ninayobaini katika usafiri huo wa umma, ni uhusiano mzuri kati ya abiria na makondakta. Siku kadhaa ambazo nimekuwa ndani ya mabasi hayo ya daladala, nimeshuhudia hali ya ustaarabu miongoni mwa abiria na makondakta.
Nikiwa kwenye daladala, pia nabaini jambo jingine; ustaarabu wa usafi wa mazingira katikati ya mji. Wakati gari likitoka kituo cha Stendi Kuu kuelekea Nanenane, binti mdogo aliyeketi karibu nami, baada ya kula mhindi wa kuchoma, anaendelea kushikilia gunzi bila kurusha nje. Takribani vituo vinne tunavyopita, yule binti anaendelea kushikilia gunzi hilo. Sikuona sababu ya kumuuliza sababu ya kulishikilia kwani ninazo taarifa kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Melkion Komba juu ya mikakati ya halmashauri kuufanya mji uwe msafi. Hivyo wananchi wana hofu kutupa taka hovyo.
Si tu utupaji taka, bali pia kuhusu upangaji bidhaa holela mitaani, ni suala ambalo Dodoma inaonekana kujitahidi ikilinganishwa na Dar es Salaam. Mtaa ninaoshuhudia wafanyabiashara wadogo ni ule ulio eneo karibu na viwanja vya Nyerere Square ambako wamepewa kibali maalumu. Dodoma ninayoiona, ni ile isiyo na msongamano wa magari.
Ni ile yenye barabara nyingi za kuchepuka. Ina barabara kuu zinazoingia kutoka Mashariki, Magharibi, Kusini na Kaskazini. Barabara hizo zinaiunganisha Dodoma na mikoa ya Manyara, Iringa, Morogoro na Singida. Hii ndiyo Dodoma yenye nidhamu. Hadi bodaboda wanasimama kwenye taa za barabarani na alama za pundamilia kupisha waendao kwa miguu. Je, nini chimbuko la ‘nidhamu’ hii? Kesho, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Melkion Komba atakuwa ana jibu.
itaendelea