Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,539
Mkuu uko sawa ila wakati mwengine wananchi wanataka kusapoti chama fulani kulingana na mwelekeo wake , ila kama ni chama cha upinzani wanaogopa kukisapoti wazi wazi kwa kuogopa kuhujumiwa.Unakuta mtu labda ni mjasiriamali; halafu akionekana anaunga mkono upinzani wanamuambia "ngoja utaona!" halafu wanaweza kumuhujumu (kumfilisi n.k.) Njia nyingine ni hii ya kuwabambika watu kesi.Sasa hali hii huwaogopesha wananchi wengi kutofautiana na chama tawala.Lakini chama chenyewe kinapoonesha mshikamano na ushirikiano, woga wa kuhujumiwa hupungua hata kwa wananchi wa kawaida wanaotaka kukiunga mkono chama kwa kuwa wanajua msaada utakapohitajika, basi, utapatikana.kwani iwe chama tawala au cha upinzani bila wananchi kukisapoti hakifiki popote.
Kwa jinsi ilivyo basi wananchi tunajukumu kubwa sana la kutoa sapoti kwa chama ili kiweze kufikia malengo
CHADEMA haijaishawishi ila JK mwenyekiti wa CCM aliiteka nyara kwa kimbelembele chake. Shukrani kubwa kwa JK maana ilikuwa ni ilani ya uchaguzi na ameitekeleza vizuri so far.Hivi Chadema ndiyo wameishawishi serikali ya CCM suala la katiba?
Hivi Chadema ndiyo wameishawishi serikali ya CCM suala la katiba?
Hivi Chadema ndiyo wameishawishi serikali ya CCM suala la katiba?
Mkuu uko sawa ila wakati mwengine wananchi wanataka kusapoti chama fulani kulingana na mwelekeo wake , ila kama ni chama cha upinzani wanaogopa kukisapoti wazi wazi kwa kuogopa kuhujumiwa.Unakuta mtu labda ni mjasiriamali; halafu akionekana anaunga mkono upinzani wanamuambia "ngoja utaona!" halafu wanaweza kumuhujumu (kumfilisi n.k.) Njia nyingine ni hii ya kuwabambika watu kesi.Sasa hali hii huwaogopesha wananchi wengi kutofautiana na chama tawala.Lakini chama chenyewe kinapoonesha mshikamano na ushirikiano, woga wa kuhujumiwa hupungua hata kwa wananchi wa kawaida wanaotaka kukiunga mkono chama kwa kuwa wanajua msaada utakapohitajika, basi, utapatikana.
Imendikwa na Elias Msuya na Freddy Azzah.12April 2011.(Vijana Forum)Hivi Chadema ndiyo wameishawishi serikali ya CCM suala la katiba?
Kimsingi mshikamano na ushirikiano wa hali ya juu "Team work" ndio nguzo muhimu zaidi ya zote kwa taasisi yeyote ile au watu wenye lengo moja na wanao pambana kuliendea lengo hilo.Ni kwa mshikamano na ushirikiano tu, watu wanaweza kulinyanyua jiwe kubwa ambalo kimsingi kama akijaribu kunyanyua mtu mmoja mmoja (mmoja baaada ya mwengine), wote wataishia kutenguka migongo na jiwe li pale pale.Ni kwa ushirikiano na mshikamano tu; Nyuki wanaweza kutengeneza asali ya kuwatosha kwa matumizi yao na nyingine nyingi ya ziada kwa matumizi ya viumbe wengine.
Mwaka 2010, CHADEMA , walishikamana na kushirikiana kweli kweli katika uchaguzi mkuu, hatimae matunda ya kazi yao yalionekana.Walifanikiwa kupata viti vingi vya ubunge kwa kiwango ambacho hakikutarajiwa.
Wabunge wa CHADEMA walishikamana ndani ya Bunge na Kuweza kuiwajibisha serikali vilivyo bungeni.Mara ya kwanza ni kipindi walivyomshinikiza Waziri mkuu El Kujiuzulu na mawaziri wengine wawili, na mara ya pili; Ni mwaka 2012 walivyoishinikiza serikali hata Rais akawajibika kupanga upya baraza la mawaziri.
CHADEMA, Kwa ushirikiano mkubwa wameendensha M4C ambayo imeonekana kuwa na mafanikio makubwa.Miongoni mwa mafanikio hayo ni kuwafanya wananchi kujitambua na hata sasa unaona CCM nayo imeenza kuzunguka hadi katika vitongoji kuwafikia wananchi (Ni jambo zuri mno) kwa kuwa washajua kuwa sasa wananchi wanajitambua sana kutokana na elimu waliyoipata kama matunda ya M4c.
Kwa kuwa CCM, wametambua silaha hii ya Mshikamano na ushirikiano ambayo imekuwa inawasaidia CHADEMA;basi wameamua kufanya kila mbinu ili kuvuruga ushirikiano na mshikamano huo.Wamekuwa wakitengeneza mizengwe kwa kuweka mapandikizi ndani ya CHADEMA, kama akina Mtela Mwampamba na timu yake .Hata hivyo kwa kutumia silaha hii hii ya Ushirikiano na mshikamano; CHADEMA wamefanikiwa kuvuka hiki kihunzi.
Kwa mshikamano wa CHADEMA, wameweza kuweka wanasheria wa kuwasimamia wanachama na viongozi wao wanaohujumiwa kisiasa na kesi zote wameonekana kuzisimamia vyema.Rejea kesi ya Lema Arusha, Kesi ya Rwakatare, Kuna yule jamaa wa Kilolo aliesweka ndani Kwa kumrekodi mkuu wa wilaya, Kuna kiongozi wa Chadema, Mtwara alikamatwa kwa kuhusiswa na vurugu za gesi na wakati hakuwepo mtwara na kesi nyengine nyingi.
CHADEMA kwa ushirikiano wao na mshikamano wao; Wameishawishi serikali ya CCM kukubali mchakato wa katiba mpya; mchakato ambao hapo awali ulipingwa na CCM.Ni kwa mshikamano na ushirikiano CHADEMA wamefanya tena vizuri na sasa mchakato unaendelea.
Hii ni mifano michache tu katika mingi.Kwa hakika Mshikamano na Ushirikiano, ni silaha imara kuliko mkuki wa chuma cha pua.Hii ndio silaha ya CHADEMA iliyowafikisha hapa walipo.Hii ndio silaha itakayo wapeleka CHADEMA hatua nyengine mbele.Maadui wa CHADEMA wataweka nguvu nyingi kuhakikisha wanaiharibu silaha hii kwa ajili ya usalama wao.Ni vyema CHADEMA wakawa na tahadhari ya ziada kuilinda silaha hii.
wameishinikiza!Hivi Chadema ndiyo wameishawishi serikali ya CCM suala la katiba?