Hii ndio Cybersquatting

Hii ndio Cybersquatting

Wazobora

Member
Joined
Jun 14, 2019
Posts
13
Reaction score
7
Cybersquatting ni nini?
- Cybersquatting ni kitendo cha kihalifu kinachofanyika mitandaoni, ambapo muhalifu wa kimtandao au mdukuzi, huchukua, hudukua au hununua jina husika mtandaoni ambapo jina hilo linamilikiwa na kampuni, mtu au biashara husika ambapo pia kwa upande mwingine huwa na hatimiliki.

Hii Mara nyingi hutokea pale Kampuni inapokuwa inahitaji kununua jina la tovuti(website domain) linaloendana na jina la kampuni na kukuta jina hilo limeshanunuliwa muda mrefu na mtu mwengine. Au kuhitaji kujiunga katika mitandao ya kijamii na kukuta jina hilo linatumika na mtu mwengine.

Wahalifu hawa hufanya ivo kwa malengo makuu manne

- Kwanza ni kuliuza jina hilo kwa gharama kubwa pindi mmiliki wa hilo jina iwe ni kampuni au mtu binafsi atakapo lihitaji kulitumia kimtandao. Mfano mzuri kwa hapa Tanzania ni blogu moja ya iliyokuwa ikitangaza wasanii wa Tanzania ya djchoka ambayo mwanzo ilikuwa ikiitwa djchoka.blogspot.com na baada ya djchoka kutaka kuibadilisha kwenda kwenye website yani djchoka.com alikuta jina hilo limesha chukuliwa tayari. Ikambidi abadili na kutumia djchokamusic.com

- Lengo la pili ni kuchafua taswira ya kampuni au mhusika mwenye jina hilo. Mfano kwa hapa Tanzania kuna wadukuzi walidukua akaunti ya Instagram ya muheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar Mhe.Paul Makonda, na baada ya kudukuliwa akaunti ile mdukuzi akapost post inayochafua wadhifa wa muheshimiwa. Na kumbidi atumie akaunti yenye jina jingine

- Lengo la tatu ni kutumia jina hilo kwaajili ya kutapelia watu. Unaweza kuona hasahasa katika mitandao ya kijamii ambako ndiko kuna jamii kubwa, jinsi matapeli wanavyotumia majina ya makampuni na watu maarufu kutapelia watu. Mfano ni matapeli waliokuwa waki watapeli watu katika mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kutumia jina la Mwanahabari maarufu nchini Millard Ayo. Na amekuwa akiwapa tahadhari watu juu ya hizo akaunti zinazo fanya utapeli kupitia instagram yake.

- Lengo la nne ni kupata umaarufu na wafuasi wengi. Leo hii kuwa na wafuasi wengi katika mitandao hasahasa ya kijamii limekuwa ni swala linalo angaliwa na kila mtu na kufanya hata wengine wafanye mambo yasiyo na maadili kupata wafuasi. Sasa wadukuzi hutumia majina ya watu maarufu ambao hawapo kwenye mitandao ya kijamii kupata wafuasi na umaarufu, na kisha baadae kuziuza either kwa muhusika ama mtu anaye hitaji akaunti yenye wafuasi wengi ili aweze kuitumia katika kutangazia biashara yake.

Kwa ufupi hiyo ndio Cybersquatting.

Makala hii inapatikana DrLitwe Blog
 
Back
Top Bottom