kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,875
Kwanza niwasalimu kwa heshima zote wanajamvi.
Kuna kipindi niliingia kwenye jopo la watu waliokuwa wanasema pesa hakuna kama ambavyo wengi wamekuwa wakisema na bado wanaamini hivyo. Ila kwasasa naamini hii ni kauli ya kisiasa ya wakosoaji wa kila kitu. Nimekuja kugundua watanzania walikuwa wanataka mabadiliko huku wakiwa hawajui nini maana ya mabadiliko. Wananchi walikuwa wanalia matumizi mabaya ya hela za serikali kwa waliopewa wajibu wa kuzitunza, miradi mibovu ,safari zisizo na tija,rushwa maeneo ya kazi n.k. Watu wakatamani sana serikali ya mabadiliko ije iyafute hayo bahati mbaya waliamini mabadiliko hayo lazima yangeletwa na Lowassa tu na kwamba wengine wasingeweza.
KWANINI PESA HAZIJAPOTEA KWA MFANYAKAZI?
Kwa mtumishi wa serikali au wa binafsi ambaye mshahara wake ulikuwa 1.5m mwaka jana bado anapokea hizo hizo hazijapungua. kwahiyo kama huyu mtumishi alikuwa anategemea tu pesa za mshahara bado hajapungukiwa. Bahati mbaya majizi yanayosema pesa imepotea walikuwa wanategemea pesa za serikali nje ya mfumo wa mshahara wao. Hali hiyo imepigwa ban wanalalama maana wanaishi kama mashetani kwasasa baada ya kukopa benki wanakokatwa mshahara wote.
HALI NI TOFAUTI KWA WAFANYA BIASHARA
Baada ya serikali kudhibiti matumizi haramu ya pesa, watu wamekuwa na uangalifu kwenye matumizi yao maana wamejikuta pesa zao hazitoshi na sasa wanaishi kwa budget. Hii hali imepunguza consumption hasa katika mambo ya anasa au mahitaji yasiyo ya lazima na hata yale ya lazima sasa yananunuliwa kwa uangalifu sana. Badala ya kupanda bodaboda kutoka mwenge hadi bamaga sasa wanapanda gari au wanatembea kwa miguu hali hii imefanya wafanyabiashara kutokuuza kama zamani na hivyo kuona pesa hakuna.
Kwa kifupi pesa halali zipo kama ilivyokuwa kawaida ila pesa za ujanja ujanja, za rushwa, za wizi, za posho zisizo na tija, za vikao visivyo na tija zilizoweka watu mjini hizo hazipo. Ndiyo maana siwashangai viongozi wa dini wanaosema hela hazijapotea na kwamba mapato yao ya kanisani yanaongezeka huenda hawa majizi hayakuwa yanasali hivyo hata kama wao hawana pesa bado waumini waaminifu wanatoa sadaka kama kawaida.
NB. KAMA UNASEMA PESA HAMNA HEBU TUPE CASH FLOW YAKO YA MWAKA JANA NA MWAKA HUU UNAOISHA TUONE WAPI PAMEPUNGUA, KAMA WEWE NI MFANYABIASHARA UJUE HIYO HALI NDIYO ULIKUWA UNAHISTAHILI KAMA NCHI INGEKUWA NA UDHIBITI WA MATUMIZI TOKA AWALI. ILA KWAKUWA HUKO NYUMA ILIKUWA HOLELA HOLELA BASI ULIKUWA UNANUFAIKA NA CHAIN YA HELA HARAMU.
(HAYA SI TU KWAMBA NI MAONI YANGU BALI NI UKWELI MCHUNGU KWA WANA CCM NA SISI TUNAOEGEMEA UPANDE WA PILI). KWASASA USIPOJISHUGHULISHA NA SHUGHULI HALALI UNAKUFA NJAA, KAMA ULIZOEA VYA KUNYONGA UNALO, KAMA ULIZOEA MATUMIZI YA ANASA IMEKULA KWAKO. KWA HILI NAOMBA HATA RAIS ASILEHEZE KAMBA AKAZE MPAKA TUJUE NAMNA YA KUPANGA BUDGET NA TUSAHAU KABISA KUWAIBIA WANANCHI.
kama una mawzo mbadala njoo na hoja, ila kwangu mabadiliko niliyokuwa hii ya kudhibiti matumizi mabaya ya kodi yangu ni mojawapo.