Hii imekaaje kwenye NDOA?

TIQO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
13,786
Reaction score
2,104
Mwanamke akiolewa na akazaa na mmewe huku mme akiwa amejenga nyumba, penzi na utamu wa ndoa unapo ingia nyongo na kufikia point ya kuachana basi utasikia mahakama inasema mgawane mali mlizo chuma wote.
Lakini mwanaume anapoteza haki ya kugawana mali pindi anapo oa mwanamke aliyemkuta na nyumba hali inakuwa tofauti hakuna kugawana mali walizo chuma wote kipindi chote cha fraha. Hii inakaaje wakuu? naombeni msaada ndugu yangu katimuliwa na mwanamke wakati wamefunga ndoa na wamezaa watoto 2. Kwa vile ana pesa basi kamtimua ndugu yangu aanzie wapi kudai kugawana mali walizo chuma wote?
 
Kiukweli Sheria ipo hivyo mali iliyopatikana lazima mgawane, kwa upande wa mwanaume akitaka anaweza kufanya hivyo, ila kiukwel kwa dume la mbegu sioni haja ya kulilia mali hizo achana nazo ingia mzigon utafanikiwa tu, wanawake wanalilia mali hizo cause wengi wao hawana future kwahiyo ndo maana wanapigania lakini kwa anayejitambua hana haja ya kufanya hivyo, embu kama ulishafanya uchunguzi angalia wale waloachiwa mali mara nyingi haifiki hata miaka mitano keshauza kila kitu na amerudia maisha ya umaskini wake,hana uchungu navyo hakutafuta yeye atajuaje kuvitunza! Maadam uzima upo na nguvu zipo aisee haina haja,inauma ndio,inachelewesha lakini utafika tu kwenye mafanikio. Kuna msemo usemao usiombe samaki omba nyavu ya kuvulia samaki na ujifunze jinsi ya kuitumia. Kama ndugu yako ni mwanaume kweli yaan asiyetaka kulelewa achane nazo afanye kazi kwa bidii atafanikiwa tu na Mungu atamsaidia.
 
Waweza kuta hata huyo mwanaume alikuwa analelewa na hana future hivyo nae hajui pa kuanzia ndio maana anadai gawiwo lake!
 
hilo nalo neno, sijawahi ona kidume akililia mali za mkewe.......wanaume wako proud, unless kama mke ndo alikuwa anamfanya atie heshima mjini......


Waweza kuta hata huyo mwanaume alikuwa analelewa na hana future hivyo nae hajui pa kuanzia ndio maana anadai gawiwo lake!
 

Ndo maana wengine wanaamua kuishi kwenye nyumba za kupanga tu ili wakiachana, kila mtu anakunja nguo zake, kwishney! Kwa sasa sheria hazipo, kumbuka, "DON'T BREAK THE LAW, BEND IT"
 
Tatizo ni pale ambapo mwanaume anakuwa tegemezi kwa mkewe ujue kuna siku ataumbuliwa tu: Hata huyo mwanamke atachoka kule mtu na ndevu zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…