Siku ingine rikodi mazungumzo yenu...na hakikisha unamuuliza jina wakati mnaanza mazungumzo ...then lazima wakulipe fidia ya mwaka mmoja bure...ukienda kwa boss wao...na yule alokujibu utumbo usitake tena kujuwa kimemkuta nini...wakikataa ilete youtube tuisambaze...
Hiyo ni biashara usipolipia wao watapata wapi hela?
Mkwepa malipo/ kodi unalalamika? Hivi ni haki kutolipia miaka miwili?
Miaka2 alafu unalalamika hivi wakati unakinunua hukujua kuwa ni cha kulipia? Sasa kila mtu akifanya kama ulivyofanya wewe huoni kuwa kampuni inaweza kufungwa kwa kukosa pesa za kuendeshea shughuli zake ikiwa pamoja na kuwalipa wafanyakazi mishahara, sisi wote ni wabahiri lakini mwenzetu umezidi 2years free! Alafu unalalamika? Usipende sana vya bure ipo siku utaenda zenji wewe, shauri yako.
Acheni kushambulia mleta Mada, hamjui local channel ni free kisheria.
Badala ya kuwalaumu star times kwa kuvunja sheria mnamnanga mleta Mada.
poleni nyie mnajua leo mimi nilishaibiwa nimelipa matangazo hamna wala sio poa jamani startimes mjirekebishe wizi gani uwoooHata mimi nimejibiwa hivyo hivyo, wametoa channels zote wamebakiza TBC tu, nimewauliza na hiyo si wangeifungia? Wanatupa wakati mgumu sana, mzazi wangu ni mjane na mstaafu hapo huangalia taarifa ya habari tu bibi wa watu. Star times wanaongeza shida kwa sie masikini, tunatoa huduma muhimu ili wazee waongeze siku zakuishi. Sasa nilipie kwangu na kwa mzazi pia, haya bwana tutajitahidi. Mwee sio bure tena? TCRA WATUDADAVULIE WALITUAHIDI NA WANAENDELEA KUSEMA LOCAL CHANELLS FREE.
Nenda kalipe miaka miwili ni mingi hebu tufuate haki tuache ubishi hata kama ni wewe ungejiskia vibaya