Nafikiri pia mchanganuo wako hauko sawa kwanini uwauze at 8 weeks? sijafanikiwakufuga wengi hivyo ila nami nawafuga. 400 wanakula mifuko 24 mpaka nimalize kuuza. Bei ya kununua ni 400*1400 = 560,000 chakula 24*50,000= 1,200,000. matumizi mengine maji umeme kijana dawa( glucose+ booster) total naweza tumia 150,000/-
Matumizi yote ni 560,000 + 1,200,000 + 150,000 = 1,910,000.
Mauzo 6,000*400= 2,400,000/- huwa napata faida between 350,000 - 450,000 na ikitokea zali nikauza kwa 6500 well then faida juu.
Ila biashara hii yataka moyo si ajabu kukuta kuku 30 wamelala asubuhi wakati usiku wote walikuwa poa
asante Mom basi hii biashara haina mzunguko wa faida..ina maana laki tatu nusu as faida ukigawanya siku 44 ambayo ni ndo hizo wiki 6 unakuta kwa suku ulikuwa unahangaikia faida ya 7000/- dah na kuku wanavyosumbua vile..mhhh hapana
We unaona hiyo Faida ndogo,kwani hiyo milioni sita ni kubwa?
We kaa nayo miezi mitatu ndani ndio utajua.
Siku hizi hakuna biashara yenye faida kubwa kama unavyofikiria,na wala hakuna biashara ya kuzemebea,lazima ujikaze mtoto wa kiume.
Anaesema anajenga kwa ajili ya mifugo ujue ananidham yapesa ya hali ya juu,sasa wewe wastan wa mwezi unaingiza pesa hiyo,na baadhi ya siku inazidi hapo hadi laki 4.Hapo umekosa nini.
La sivyo,nunua bodaboda ukajimalize,maana kwa ulivyo huko ndio kutakutoa roho.Biashara uvumilivu kaka
Hahahaha,Wiseboy huo sio ushauri wala sio Dongo.duuuuuh sijaelewa umenipa madongo au ushaur
mkuuu yan imenistua sana hii bsness...lakini mbona watu wanaikimbilia eti maraa ooh nimejenga kwa broilers
Hizi hesabu zako nadhani zipo too theoretical , mimi nafuga broilers kwa week4-5, hesabu yangu ya total expenditure ni 350,000-370,000 kwa kila kuku 100 na total turnover ni 100'000-130'000. Hii calculator haijawahi kuniaibisha
Nafikiri pia mchanganuo wako hauko sawa kwanini uwauze at 8 weeks? sijafanikiwakufuga wengi hivyo ila nami nawafuga. 400 wanakula mifuko 24 mpaka nimalize kuuza. Bei ya kununua ni 400*1400 = 560,000 chakula 24*50,000= 1,200,000. matumizi mengine maji umeme kijana dawa( glucose+ booster) total naweza tumia 150,000/-
Matumizi yote ni 560,000 + 1,200,000 + 150,000 = 1,910,000.
Mauzo 6,000*400= 2,400,000/- huwa napata faida between 350,000 - 450,000 na ikitokea zali nikauza kwa 6500 well then faida juu.
Ila biashara hii yataka moyo si ajabu kukuta kuku 30 wamelala asubuhi wakati usiku wote walikuwa poa
Hizi hesabu zenu bado zinanipa shida sana mkuu..Nikirudi kwa mleta uzi Wiseboy, ushauri alikupa Zanzibar Spices nakubaliana nao. Kila mtu.ana staili yake ya kushauri. Nami najenga frame za biashara kwa biashara hii hii ya kuku broilers. Ingawa napata changamoto ya kulaliwa bei ya kuku at the end of the day. Ila sikati tamaa wala siachi kufuga. Kwanza kabisa huo.mchanganuo wako si wa kweli. Bado hujafanya research vzr. Bei ya juu ya kifaranga ni 1400, interchick. Nimenunua leo vifaranga vya Mkuza kwa 1000/-. Chakula cha kuku ninachotumia hakizidi elfu 43. Kuku wanauzwa kuanzia wiki ya 4-5. Kwa sasa huwa naweka kuku batch 2, elfu 1 vifaranga na elfu 1 wakubwa. Ila nilianza na kuku 400 na walikuwa wanatumia mifuko km 26. Mahesabu ya Mom nakubaliana nayto. Fanya hesabu km kuku 400 mifuko 24, kuku 1000 mifuko mingapi. Na pia kutokana na soko wakati mwingine ni changamoto, kwa wewe unayeanza sikushauri uanze na 1000. Anza angalau na 500
Mkuu Mom msaada kwenye tuta, hiyo naonba uniunganishe na wateja wako wa kuku. Hao wanaonunua mmoja kwa elfu 6. Natanguliza shukran