cpu na gpu
mkuu kuna kitu inabidi ukifahamu kwanza, kuna njia mbili za kurender video ambazo ni kwa kutumia cpu na gpu
-kutumia cpu utahitaji cpu yenye core nyingi na yenye nguvu na huchukua muda mrefu, pia njia hii ndio hutumiwa na kampuni kubwa za video editing na pia computer zake zina gharama. output yake ni video yenye quality kubwa sababu makosa yanakuwa madogo
-kutumia gpu ni njia ya haraka sana, hasa gpu za nvidia zenye cuda, gpu za bei rahisi kama gtx 750ti ina core 640 za cuda software za video editing zinapenda core nyingi hivyo kazi inaisha mapema. output yake mara nyingi video haiwi na quality kama ukitumia cpu, sema inaweza kuwa quality inayotosha kwa matumizi yako. ipo njia nyengine ya kutumia gpu zinazokuja na processor za intel yaani intel hd graphics, njia hii ina speed kushinda hata cuda ya nvidia lakini si software zote zinasuport na kwa bahati mbaya adobe ni mmoja wapo wa kampuni zisizosuport gpu za intel hd (quicksync)
kutokana na hapo sasa tunapata chaguzi nyingi
1. zidisha kidogo budget tafuta mashine yenye core i7 5820k hii cpu ina core 6 na thread 12 halafu tafuta na gpu ya kawaida kama gtx 750ti, utaipata around dola 1,000 hadi 1200 hivi . computer hii hutakuwa na mawazo pro wengi duniani wanatumia hio cpu.
2. tumia cpu za amd kama fx 8350 core zake hazina nguvu lakini ina core 8 kwa bei rahisi, halafu tumia gpu kama 750ti tena. computer hii itacost around dola 500 hadi 600 watu wengi wanaofanya video editing wakiwa na budget ndogo hutumia hii processor. hii cpu inacompete na i7 na inazipita latest i3 na i5 kwenye video editing.
3. piga moyo konde nenda gpu rendering, tafuta pc yenye cpu ya kawaida halafu eka gpu nzuri. unaweza kwenda machinga complex desktop za i3 second generation ni around 300,000 halafu nunua gtx 750ti ebay around 200,000 utapata mashine ya kuanzia around 500,000.
cheki hii graph hapa itakusaidi
http://media.bestofmicro.com/6/1/516025/original/adobecc-media-encoder.png
mambo mengine tofauti na cpu na gpu
1. storage
kwenye video editing si lazima uwe na ssd ila sio mbaya ukiwa nayo itakusaidia kwenye kulaunch software faster, computer kuwaha haraka etc. cha muhimu kwenye video editing uwe na hdd mbili na uzitengenezee raid. raid inamaanisha unakuwa na hdd mfano zote zina 1tb halafu zinasync muda wote, kila kilicho kwenye hdd moja kinakaa kwenye hdd nyengine na badala ya kuwa na 2tb itabaki ile ile 1tb japo zipo mbili. hii huongeza sana speed na hata adobe wenyewe wameirecomend.
2.ram
kadri utakavyoweza kununua, ni vyema pia motherboard yako ikawa na slot 4 kama utaamua kununua 5820k na kuanzia slot 2 kwa hizo cpu nyengine. processor za siku hizi zinatumia ram zaidi ya moja kuboost speed (dual chanell/quad chanell) hivyo kama unaamua ram iwe 16gb basi hakikisha zinakuwa ni 8gb mara mbili.
3.monitor
kwa perfomance nzuri nunua monitor yenye technology ya gpu yako, mfano umenunua gtx 750ti yenye g-sync hakikisha na monitor nayo ina hio technology, husaidia sana kufanya kinachooneshwa kwenye monitor kuwa smooth bila lag wala tearing