Mkuu, usiiuze. Jichange ufunge engine ya Diesel na hutogombana tena na madereva. Hiace ni gari ngumu. Hapo ilipo inaweza kuendelea kukuzalishia kwa miaka mingine nane. Cha kufanya ipeleke ruti fupi. Nina uzoefu na hii biashara. Ukipeleka ruti ndefu pesa inakuja lakini nyingi inarudi kwenye matengenezo. Ukiipeleka mfano ipige ruti za Mwanza mjini pale (au Tanga mjini) unaweza ukapata elfu arobaini na tano hadi hamsini kwa gari ya Petrol lakini pia matengenezo yanakuwa ni madogo so unaiona pesa yako.
Ukiiuza hiyo gari pesa utakula ndani ya mda mfupi zitakuwa zimekwisha ila ikiendelea kuzalisha kwa miaka mingine nane, utakua umenunua nyingine kama hizo mbili...