HESLB yakanusha taarifa zinazosambazwa mitandao ya kijamii kuhusu vigezo vya kupata mikopo

Sadick Nkinda

Member
Feb 15, 2014
77
9
KUKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KUPITIA MITANDAO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na mara mchakato utakapokamilika, wadau wote watatangaziwa.

Mwisho.

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016

HESLB.JPG
 
Taratibu zinazosubiriwa kukamilishwa ni pamoja na hivyo vigezo vya mkopi kukopeshwa, haitakuwa ajabu hatimaye tukajua kuwa walikanusha muda wa toleo la tangazo na sii maudhui.

Ujinga ujinga huu enzi hizo Mungu hakuuvumilia kabisa!! Angesha lipua moto akaanza upya.
 
Tcu inaendeshwa kisiasa Sasa kila Mwaka kanuni mpya, wakati nchi ni Ile Ile
Inatia hasira sana, mnawatesa watoto wa maskini wanaosoma kwa shida kuanzia chekechea mpaka secondary
 
Lakini Siku Zote Rumors Ndiyo inayoukaribisha Ukweli!
Haya Tunasubiri Natuone!
 
BODI YA MIKOPO YAKANUSHA KUTOA VIGEZO VYA MIKOPO 2016/17

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Bodi hiyo inapinga taarifa zinazosambazwa ambazo pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma na kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Jerry Sabi amesema taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wadau wote wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Bodi ya Mikopo yakanusha kutoa vigezo vya mikopo 2016/17
 
KUKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KUPITIA MITANDAO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na mara mchakato utakapokamilika, wadau wote watatangaziwa.

Mwisho.

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016

Hawa ni wezi tu hawana lolote. Tunataka tufahamu ilikuwaje wakatoa mikopo kwa form four wa st. John's university.
 
KUKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KUPITIA MITANDAO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na mara mchakato utakapokamilika, wadau wote watatangaziwa.

Mwisho.

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016

mpaka mupate kauli ya rais ndio muanze new applications this is too much.,
 
HAWANA LOLOTE HAO WANASEMAGA TU HVYO MWISHO WA SIKU NDO INAKUWA HVYO KAMA UNA KUMBUKA ILE ISHU YA KUPANDISHA VIGEZO VYA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU MWANZO TAARIFA ZIKAJA KAMA HV HALAFU WAKATOKEA NA KUANZA KUSEMA TUNA KANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA NI UZUSHI SUBIRI MPKA TUTAKAPO TOA TAARIFA KAMILI MWSHO WA SIKU WANAKUJA KUTOA TAARIFA YAO NI YALE YALE YALIYOKUWA YANA SAMBAZWA KWAHYO KUWENI MAAKINI MAANA NI SAWA NA PANYA ANAYEKUNG'ATA HALAFU ANAKUPUULIZA MWISHO WA SIKU MAUMIVU YALE YALE .......TANZANIA BWANA HELA YENYEWE NI YA MKOPO MASHARTI YA NINI SASA JE WANGEKUWA WANATOA BURE INGEKUWAJE....????
 
Umeangalia tarehe ya kutumwa kwa post uliyocomment?!
 
Back
Top Bottom