HESLB wamekuwa matapeli ama vipi?

HESLB wamekuwa matapeli ama vipi?

MKEHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
716
Reaction score
1,144
Hawa ndugu zetu wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu siwaelewi. Wakiwa wanakudai kila siku wako mlangoni kwako na kama umeajiriwa kila siku unao ofisini kwako.

Hiyo yote ni kuonyesha how serious they are. Shida inakuja unapomaliza deni lako na ukawa umewalila zaidi kwa maana ya OVER PAYMENT ukawa unawadai wao utasumbuliwa ukiwa na roho ndogo mpaka utakata tamaa na hela utawaachia.

Utaambiwa ujaze form na uweke viambata ambavyo utakoma kuvitafuta. Utaambiwa mfumo uligoma kidogo tunaufanyia matengenezo mpaka kero. Wakati mnatudai kiroho safi mlichukua hela zetu kwenye mishahara yetu mpaka interest mkakomba na jambo lenu lile la RETENTION tulikaa kimya mpaka Mheshimiwa rais Ndugu Samia Suluhu Hassan akatuknea huruma wananchi wake akalitoa tunamshukuru sana kwa hilo.

Sasa iweje leo mwaka wa pili nawaomba hela zangu ambazo ni jasho langu halali hamnipi hela yangu. Kama ni form ya mtandandaoni mmenijazisha sana mara tuma koambata hiki mara kile jamani nirudisheni hela zangu halali mlishachukua chenu nilirudisheni changu.

Yaani zaidi ya nusu milioni mmeshikilia hamjui kama ni Hela ya milango mitatu kabisa hiyo ama mpaka tuperekane kotini? Mkipigiwa simu hampokei simu mmeweka kama bosheni tu. Au mnataka nitoke huku Buhigwe niwaduate TAZARA DAR ndo mjue mnatunyima haki zetu?

Kama mnavyo harakisha kukata mishahara yetu harakisheni na kurupa hela mlizochukua kimakosa kutoka kwenye vibubu vyetu.
 
Pole mkuu
Siwatetei BODI YA MIKOPO, ila nasema fact... Niliweka viambatanisho vyote na walinilipa ndani ya siku 90 overpayment yangu. Sikupata shida nao kabisa na wapo 'honesty' kulipa.
Fuatilia tena usichoke, lazima kuna kitu hakipo sawa.
 
Asante kwa kunitia moyo
 
Hawa ndugu zetu wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu siwaelewi. Wakiwa wanakudai kila siku wako mlangoni kwako na kama umeajiriwa kila siku unao ofisini kwako. Hiyo yote ni kuonyesha how serious they are. Shida inakuja unapomaliza deni lako na ukawa umewalila zaidi kwa maana ya OVER PAYMENT ukawa unawadai wao utasumbuliwa ukiwa na roho ndogo mpaka utakata tamaa na hela utawaachia.
Utaambiwa ujaze form na uweke viambata ambavyo utakoma kuvitafuta. Utaambiwa mfumo uligoma kidogo tunaufanyia matengenezo mpaka kero. Wakati mnatudai kiroho safi mlichukua hela zetu kwenye mishahara yetu mpaka interest mkakomba na jambo lenu lile la RETENTION tulikaa kimya mpaka Mheshimiwa rais Ndugu Samia Suluhu Hassan akatuknea huruma wananchi wake akalitoa tunamshukuru sana kwa hilo.

Sasa iweje leo mwaka wa pili nawaomba hela zangu ambazo ni jasho langu halali hamnipi hela yangu. Kama ni form ya mtandandaoni mmenijazisha sana mara tuma koambata hiki mara kile jamani nirudisheni hela zangu halali mlishachukua chenu nilirudisheni changu. Yaani zaidi ya nusu milioni mmeshikilia hamjui kama ni Hela ya milango mitatu kabisa hiyo ama mpaka tuperekane kotini? Mkipigiwa simu hampokei simu mmeweka kama bosheni tu. Au mnataka nitoke huku Buhigwe niwaduate TAZARA DAR ndo mjue mnatunyima haki zetu? Kama mnavyo harakisha kukata mishahara yetu harakisheni na kurupa hela mlizochukua kimakosa kutoka kwenye vibubu vyetu
Ni mijitu mipuuzi na majizi Sana! Mimi yakinizungusha natafuta wakili watalipa na fidia, mbuzi Sana!
 
Huo muda wa siku 90 uliowekwa kisheria bado ni mrefu mno kwa bodi kumrudishia mtu hela ambayo hakunufaika nayo au alikatwa kimakosa.Kama kungekuwa na watu wenye hofu ya Mungu hapo bodi ya mikopo ya elimu ya juu siku 3o zinatosha kumrudishia mtu hela zake.Ajabu mtu akijaza online refund hakuna anayejali wala kuona umuhimu wa kushughulikia .
 
Back
Top Bottom