HESLB tunaomba ufafanuzi

HESLB tunaomba ufafanuzi

Enzymes

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
4,332
Reaction score
3,018
Natambua kuwa taasisi hii haina uongozi wa ngazi za juu hadi sasa baada ya vigogo wake kutumbuliwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo wizi ulio kubuu na uendeshaji wa taasisi usio ridhisha.

Ni waombe mliopo mtupe ufafanuzi kwa haya machache:

1. Ni nini tofauti ya Retention fee na PENALTY? Uelewa wangu ni kuwa Penalty in kava hadi retention fee (money value retention). Hata benki hutoza riba ambayo kwa ndani ina retention fee, uwezekano wa mkopaji kutorejesha mkopo, faida yao (return), nk. Iweje penalty yenu iwe sawa na retention fee? i.e 5% @

2. INVOICE (BILL ) zenu asilimia kubwa ni za kugushi haziendani na jumla + penalty+ the so called retention fee. Mtu anakuwa na bill kubwa kuliko alichotumia. Mf. Bill mliomletea mtu chuoni inaonesha Tshs 7M baada ya miaka 4 bill yake mliyoleta kazini inasoma Tshs 16M!! Hivi mnafumba macho na kubandika namba au ndio mnataka kufidia utumbuaji wa Ndalichako na wanafunzi hewa mliokuwa mnawaongezea vyuo ili hali vyuoni hawapo?

3. Kama jumla ya mkopo wa mkopaji ni Tshs 7M na baada ya miaka 4 inakuwa Tshs 16M, je hii ni mikopo ya kusaidia watoto wa maskini au ni uhuni? Je riba na penalty zenu ni special sana tofauti za Benki kama CRDB ,nk au? Je riba zingekuwa hivi mnadhani kungekuwepo na mkopaji ktk mabenki?

4. Kuna utofauti mkubwa sana kati ya watu wa miaka ya 2000 na miaka ya 2005 na kuendelea. Wao walikuwa wanakatwa Tshs 15,000 au Tshs 25,000. Kwa sasa kuna watu wanalkatwa hadi Tshs 150,000 na kuendelea, 10% kulingana na mshahara wako. Je meals, accommodation na field zilikuwa part ya allowance (subsidize) au ni part ya Loan?

5. Je ni kwann mchaji watu penalty ya 10% wakati katika mkataba (fomu) mliosaini kipengele hicho hakikuwemo awali?

6. Mnatumia kigezo gani cha kuanza kutoza faini ya uchelewaji wakati nyie binafsi na serikali yake hamna soko bora la ajira? Je mnafahamuje kuwa huyu mhusika kwa sasa kashapata kazi ila hataki kulipa tu hivyo anastahili penalty? Muache mambo ya uganga wa kienyeji hapa!! Hiyo faini muifute. Hii ni Gvt money, lengo lake ni kuwezesha watanzania wote kwa usawa kufikia elimu ya juu na si kugeuza mikopo hii kama biashara kwenu na kushindana na mabenki!! Benk zenyewe ni Reducing Balance, mkopo wenu ni Constant wapi na wapi? kama hamjui mambo kwann msiwaone Benki?

7. Ni kwann wanachuo wengi wa miaka ya nyuma waliopata multiple selection mmewajazia INVOICE za chuo moja wapo hasa chenye ADA kubwa?

8. Mnao lipa kwasasa mikopo ya HESLB nendeni mkahakiki mikopo yenu. Madeni mnayo lipa mengi siyo. Kuna watu wana INVOICE hadi za miaka 4 ili hali wamesoma miaka 3, kuna watu wamewekewa Tshs 16M ili hali wamesomea Tshs 7M.

9. Najuiuliza hiyo Tshs 16M kwa Mwl wa Mshahara wa Tshs 500,000/=. 10% ni Tshs 50,000. Je Tshs 16M atailipa kwa muda gani? Ni sawa na miezi 320 amabayo ni wastani wa miaka 27!! Si atakuwa amekufa? Au amestaafu!! Au mtakata na NSSF /PENSION yake?

Ombi langu: Msifananishe hii mikopo na mikopo ya kibiashara. Hii ni sawa na Mikopo au misada ya TASAF.

Ni hayo tu. Nawaombeni ufafanuzi wenu.
 
Back
Top Bottom