Bishop Mafie
Member
- Apr 10, 2015
- 24
- 9
Ndugu Mpendwa,
Amani iwe nawe! Tunamtukuza Mungu kwa Mwaka Mpya 2018.
Tumeona miaka ikianza na kumalizika kwa kadiri Mungu atupavyo neema. Suala la msingi ni kutafakari pia 'tunawaza nini juu ya BWANA', katika maisha yetu; *Kuinuliwa, kutiwa nguvu zaidi, kufanikiwa, au kubarikiwa, na hatua nyingi zaidi, pamoja na yote yatakayoujaza Mwaka Mpya, tujiulize na kuona kuwa tuna majibu mazuri ya kile tunachowaza juu ya BWANA*. (Tazama: NAHUMU 1:9)
Ni vema katika yote, ghala, hazina zetu, na vingine vingi, vyote vyenye kutupa hatua mbele zaidi, tujihakiki kuwa tunawaza vema juu ya BWANA, *kukaa uweponi mwake, kuimarisha mahusiano na Yeye, kujawa na bubujiko la Roho Mtakatifu zaidi, na mengine mengi yaliyojaa uchaji ili kumpendeza Mungu zaidi*, kila siku katika Mwaka 2018.
Tuchague kuwa katika fungu la wenye busara na sio wapumbavu, na hasa mbele za Mungu. *Mwaka 2018 zaidi uwe wa kwetu 'kujitajirisha kwa Mungu' na sio nafsi zetu wenyewe*. (Tazama: LUKA 12:16-21).
*Nakutakia utele wa baraka, amani, furaha, upendo, na mengine zaidi na zaidi*, na hasa Mungu kuwa pamoja nawe wakati wote katika Mwaka 2018.
Kwa niaba ya wote katika WIN ALL FOR CHRIST (WAC), nakutakia,
*HERI YA MWAKA MPYA, 2018!*
*(HAPPY NEW YEAR, 2018)*
Michael Mafie
E-Mail: <mafie@wacinternational.org>