Wana bodi,
Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mungu kwa ajili yako nami, kupewa neema ya uzima tuendelee kumtumikia katika mwaka huu mpya wa 2013 kwa kadri ya siku atakazotujalia tumtumikie katika mwaka huu.
Pamoja na milima na mabonde tulopitia mwaka ulopita lakini tunapaswa kumshukuru Mungu kwa yote. Maisha ndivyo yalivyo. Hakuna mwaka mzuri wala mwaka mbaya. Mungu kaiweka yote kwa ajili yetu wanadamu tujue kuwa Mungu yupo hai na anafanya kazi yake maishani mwetu.
Basi nawatakieni kila lililo la heri kwa mwaka huu, Mungu awafanikishe matamanio ya mioyo yenu mwaka huu 2013 :israel: