From Wikipedia...
Martin alizaliwa mjini
Atlanta,
Georgia,
Marekani. Alikuwa mtoto wa mzee Martin Luther King Sr. ambaye pia alikuwa mchungaji na kiongozi wa kupigania
haki za binadamu. Baba yake alimwita
Martin Luther ili amheshimu huyu
mtaalamu Mjerumani wa
karne ya 16.
Aliwaongoza Waamerika Weusi kupinga
ubaguzi wa rangi uliokuwepo katika sehemu za USA mpaka
miaka ya 1960. Katika mapambano hayo alifuata mapokeo ya
Mt. Agostino katika
Kanisa. Alieleza ya kuwa kila
mtu amepewa na
Mungu heshima yake, hivyo
sheria za nchi na
serikali zinazovunja heshima hiyo si za haki. "Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu" (
Mdo. 5:29).
Aliwaita watu kupinga
ubaguzi hata dhidi ya serikali na
polisi lakini bila kutumia mabavu. Watu waliongozwa na M. L. King
waliandamana mahali pengi wakanyamaza wakipigwa na kukamatwa. Wakaingia katika
hoteli,
shule na
vyombo vya usafirivilivyotengwa kisheria kwa watu weupe, wakasubiri mpaka polisi ilipoitwa na kuwakamata. Wakapokea
adhabu na mapigo.
Baada ya miaka kadhaa mapambano kwa silaha hizo za
amani yalishinda.
Mahakama kuu ya Marekani na serikali kuu zilitangaza ya kuwa ubaguzi wa rangi katika mikoa mbalimbali hauruhusiwi kuendelea.
Mwaka
1964 alipokea
Tuzo ya Nobel ya Amani kwa sababu ya kutetea haki bila ya kutumia mabavu.
Hata hivyo aliuawa kwa kupigwa risasi na mteteaji wa ubaguzi wa rangi mwaka 1968.
Baada ya hapo
ujumbe wake ulizidi kukubalika na sheria mbalimbali zilibadilishwa.
Anahesabika kama mmoja wa watu wakubwa wa
Mungu katika
historia ya Kanisa.