Heko idara vyuo vikuu kwa kukuza viongozi

Heko idara vyuo vikuu kwa kukuza viongozi

Omary Kipingu

Member
Joined
Feb 22, 2016
Posts
40
Reaction score
48
HEKO IDARA VYUO VIKUU

Uongozi hujengwa na vitendo vya kujenga viongozi wengine, kiongozi asiyeweza kujenga viongozi wengine hafai kuwa kiongozi Bali kiongozi anayetengeneza mazingira ya kujenga viongozi wengine Huyo ndio kiongozi.

Idara ya Vyuo vikuu chini ya uongozi wa comrade Daniel Zenda inadhihirisha nini maana ya uongozi kwa kujenga mazingira bora kwa kutengenezea viongozi wengine. Msimamo wa viongozi idara ya Vyuo vikuu unatoa Dira chanya kwa mustakabali wa chama na serikali kwa kizazi kijacho.

Zenda ndiye sehemu ya wachache wenye msimamo tumpe support, ataisaidia UVCCM, iliyomomonyoka kimaadili, isiyokuwa na mtazamo wa mbele zaidi kwa sasa. Makundi yaliyopo yanayojengwa na watu wenye fikra ya maslahi ya wachache. Ambayo hata mh. Rais yanamuumiza moyo wake. Viongozi kama hawa akina zenda nikimjumuisha na Ndg. H. Polepole ni viongozi wachache wa kariba Hii kwa vijana.

Vijana wa sasa tunapenda maendeleo ya nchi yetu tuna mifano mingi ya kuiga kwa viongozi wazuri kama hawa. Chama cha mapinduzi hakiwezi kamwe kuendelea kuwa sehemu ya maficho ya wanyang'anyi na wapiga dili, tumeamua kujisahihisha tulipokosea ili kuwa na mwanzo mzuri. Nanukuu maneno ya Rais J. Magufuli "vijana wa CCM walishakuwa na makundi na ss tuanze upya" hii ni kauli yake pale Mwl. J.Nyerere memorial. Kigamboni. Ushauri huu usipuuzwe hata kidogo. Tujitathimini na tuanze upya. Asanteni.

Mtazamo hoyeeeee!!!!

By Green hybrid.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Li Polepole siyo likijana hilo! Limezeeka sura kama mimi!
 
Back
Top Bottom