Heko Agrey D. Mwanry

Heko Agrey D. Mwanry

raia_mwema

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
479
Reaction score
314
Miongoni mwa mawaziri bora Tanzania ukiacha Mwakyembe na Magufulu huyu mh. Mwanry ni mchapakazi bora sana yupo serious na ni hodari katika utendaji wake.

Sasa hivi yupo katika taarifa ya habari ya ITV anaonekana katika ziara yake huko Shinyanga.
 
Hamna ubora hapo..huwa anajifanya mkali kumbe ni usanii wa Nditta.kwanza huyu ni Gamba gumu kabisa
 
ni miongoni mwa viongozi wa CCM anayeniburudisha.. nampenda kwa hilo, wengine hata uongo wao unakarahisha
 
Miongoni mwa mawaziri bora Tanzania ukiacha Mwakyembe na Magufulu huyu mh. Mwanry ni mchapakazi bora sana yupo serious na ni hodari katika utendaji wake.

Sasa hivi yupo katika taarifa ya habari ya ITV anaonekana katika ziara yake huko Shinyanga.

Amefanya nini?
 
kama kwako kufanya ziara ndio uchapakazi basi umepotea. mtu hapimwi kwa ziara bali kwa matendo yake- yaani kitu gani amefanya ambacho kimetatua matatizo ya wananchi na sio ziara, kwani hawajaanza kufanya leo, kila siku zinafanyika na nchi bado maskini
 
Amefanya nini?

jamaa kwa kupiga mkwara hajambo. hata mimi namuona kama mzuri, ila sina detail kuhusu ufisadi. kama kuna mtu anazo data aje nazo hapa, otherwise jamaa yuko vizuri. kwani mkuu wewe ulitaka afanye nini?
 
Miongoni mwa mawaziri bora Tanzania ukiacha Mwakyembe na Magufulu huyu mh. Mwanry ni mchapakazi bora sana yupo serious na ni hodari katika utendaji wake.

Sasa hivi yupo katika taarifa ya habari ya ITV anaonekana katika ziara yake huko Shinyanga.

Si huyu anayebeba MKEWE KWENYE safari zake na pia kuhutubia ili kupata PerDeM as well... Sijawahi kuona hivyo ni Rais KIKWETE huwa anamtumia Mama Salma kuhutubia wananchi wakati wa SHEREHE za CCM KIGOMA

Sasa Kama Uchapakazi ni kutumia MKEWE pia MORE POWER 2 HIM; Enzi za JK NYERERE wake Walikuwa na HESHIMA sio kuburutwa kuchota PESA za KODI za wananchi na NCHI ni MASIKINI

*** SOMA CHINI***

2/13/13 Mke wa Waziri Mwanri afichua siri ya mumewe

www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/8220-mke-wa-waziri-mwanri-afichua-siri-ya-mumewe?tmpl=component&print=1&layout=default&page= 1/1

MKE WA WAZIRI MWANRI AFICHUA SIRI YA MUMEWE

KUFUATIA Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri kuwa mkali na kukagua ujenzi wa miradi ya kijamii mkoani Rukwa kwa umakini mkubwa na kubaini mapungufu mengi mkewe Agnes Mwanri amefunguka na kusema ndivyo alivyo hata akiwa nyumbani kwao.

Mama Mwanri anafuatana na mumewe katika ziara ya kikazi ya siku sita mkoani hapa.

Alisema: ‘’Msimshangae mkadhani anajipendekeza hapana yeye (Mwanri) ndiyo alivyo hata akiwa nyumbani
anafanya vitu vyake kwa umakini wa hali ya juu na hapendi kudanganywa wala kuona watu wakidhulumiwa haki zao.

‘’Mume wangu ndivyo alivyo hata akiwa nyumbani kwanza hapendi uonevu wala udanganyifu wa aina yoyote ile yeye siku zote anasimama katika haki.

Hivyo nimeamua kuwaeleza haya kwa sababu kutokana na kuwa makini katika kazi zake hususani anapokagua ujenzi wa miradi, isieleweke kuwa anajipendekeza la hasha yeye ndivyo alivyo,’’ alisema.

Mwanri amekuwa kivutio kikubwa na kumwagiwa sifa kemkem na wananchi katika maeneo mbalimbali alipotembelea na kukagua ujenzi wa miradi ya kijamii wakidai kwamba hawajawahi kushuhudia kiongozi yeyote wa ngazi za juu akikagua ujenzi wa miradi hiyo kwa umakini wa hali ya Juu.
 
Anazuga tu,alijua kuna kamera za itv akajifanya mkali mara aingie kwenye mtaro
 
jamaa kwa kupiga mkwara hajambo. hata mimi namuona kama mzuri, ila sina detail kuhusu ufisadi. kama kuna mtu anazo data aje nazo hapa, otherwise jamaa yuko vizuri. kwani mkuu wewe ulitaka afanye nini?

Nilitaka afanye zaidi ya kupiga mkwala ili aitwe amefanya vizuri.

Nchi haiendeshwi kwa mikwala.

Na mabaradhuli waskishtukia waziri kazi yake ni kupiga mkwala watatumaliza.

Hata watoto wa siku hizi hawa respond kwa mkwala.
 
Ha ha ha..! Eti mikwara ya "ndita"!!! Mwanry upoooo!
This is JF bhana, hakuna mfano.
 
Si huyu anayebeba MKEWE KWENYE safari zake na pia kuhutubia ili kupata PerDeM as well... Sijawahi kuona hivyo ni Rais KIKWETE huwa anamtumia Mama Salma kuhutubia wananchi wakati wa SHEREHE za CCM KIGOMA

Sasa Kama Uchapakazi ni kutumia MKEWE pia MORE POWER 2 HIM; Enzi za JK NYERERE wake Walikuwa na HESHIMA sio kuburutwa kuchota PESA za KODI za wananchi na NCHI ni MASIKINI

*** SOMA CHINI***

2/13/13 Mke wa Waziri Mwanri afichua siri ya mumewe

www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/8220-mke-wa-waziri-mwanri-afichua-siri-ya-mumewe?tmpl=component&print=1&layout=default&page= 1/1

MKE WA WAZIRI MWANRI AFICHUA SIRI YA MUMEWE

KUFUATIA Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri kuwa mkali na kukagua ujenzi wa miradi ya kijamii mkoani Rukwa kwa umakini mkubwa na kubaini mapungufu mengi mkewe Agnes Mwanri amefunguka na kusema ndivyo alivyo hata akiwa nyumbani kwao.

Mama Mwanri anafuatana na mumewe katika ziara ya kikazi ya siku sita mkoani hapa.

Alisema: ‘’Msimshangae mkadhani anajipendekeza hapana yeye (Mwanri) ndiyo alivyo hata akiwa nyumbani
anafanya vitu vyake kwa umakini wa hali ya juu na hapendi kudanganywa wala kuona watu wakidhulumiwa haki zao.

‘’Mume wangu ndivyo alivyo hata akiwa nyumbani kwanza hapendi uonevu wala udanganyifu wa aina yoyote ile yeye siku zote anasimama katika haki.

Hivyo nimeamua kuwaeleza haya kwa sababu kutokana na kuwa makini katika kazi zake hususani anapokagua ujenzi wa miradi, isieleweke kuwa anajipendekeza la hasha yeye ndivyo alivyo,’’ alisema.

Mwanri amekuwa kivutio kikubwa na kumwagiwa sifa kemkem na wananchi katika maeneo mbalimbali alipotembelea na kukagua ujenzi wa miradi ya kijamii wakidai kwamba hawajawahi kushuhudia kiongozi yeyote wa ngazi za juu akikagua ujenzi wa miradi hiyo kwa umakini wa hali ya Juu.

Mwizi na fisadi tu huyo kaja mpanda na kuziacha na umaskini mkubwa halmashauri zote mbili alipanga zaira ya siku 3 ila akaongeza huku huku na kukaa wiki nzima tena alipangiwa vyumba viwili kwenye hotel ya lyamba lyamfipa akakataa akaenda kukaa hotel moja ya kifahari katika mbuga ya wanyama ya katavi kwa siku 4 huku akiwa ameripiwa vyumba viwili lyamba lyamfipa chake na cha mkewe vyenye thamani kubwa na walishalipia kwa siku zote pamoja na chakula pia yeye na mkewe walipanda magari mawili tofauti na msafara ulikuwa mkubwa gharama zote zikilipwa na halmashauri.Alilazimisha safari ya kwenda katika tarafa ya mwese sababu kuna wachaga wenyake.Anapenda kugombeza na kuongea kwa jazba bila sababu ya maana ila wenzie wanamuenjoy 2!!Naomba mnisaidie je ziara za mawaziri mikoani huwa inalipiwa na nani?
 
jamaa kwa kupiga mkwara hajambo. hata mimi namuona kama mzuri, ila sina detail kuhusu ufisadi. kama kuna mtu anazo data aje nazo hapa, otherwise jamaa yuko vizuri. kwani mkuu wewe ulitaka afanye nini?

Kwweli kabisa! Jamaa kwa Mkwara ni Hodari na zungumza yake ni ya hisia kali sana lakini undani wake HOVYO! Anakula ruhswa ni hakuna!

Subiri huko Shinyanga atakapopewa cha juu tu, Kimya! na huko ndo tumesikia mabilioni yameteketezwa.
 
Hana lolote, anataka aonekane mchapa kazi lakini naona maneno mengi bila vitendo. CCM kuna mawaziri wawili tu wachapa kazi na huwa hatuwaoni wakiongea sana bali tunaona vitendo vyao ie Magufuli na Mwakyembe.
 
ana biti za apa na pale ila huwezi mweka the same class na majembe hayo uyu ni kijiko tuu
 
Mwanri ni sanaa namba mmoja anachimba bit tu na huenda anakula rushwa. Nani aliwahi kuchukuliwa hatua na Mwanri? Hata mtendaji wa kijini hajawahi kumfukuza kazi. Yeye hana tofauti na JK wanapendwa na kila mtu
 
Back
Top Bottom