Hekima 10

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,552
Reaction score
59,391
Hekima 1
Unaweza kuwa kiongozi mzuri bila kuanika madhaifu ya mtangulizi wako Rekebisha kwa kadri unavyoweza matendo yatasema yenyewe.

Hekima 2
Unaweza kueneza Imani yako bila kuisema vibaya Imani ya watu wengine. Elezea uzuri wa imani yako wakivutiwa watakuja wenyewe.

Hekima 3
Usitafute mafanikio kwa kumkosesha mwingine. Dunia haijawahi kuishiwa kitu cha kumhudumia kila mtu kwa sababu hata mwenye vingi akiondoka anaacha vyote.

Hekima 4
Mchawi akija kwako bila kuonekana usimuangamize kwa kuonekana. Ukifanya hivyo wewe ndio utakuwa mhalifu na yeye mwenye haki.

Hekima 5
Usifikiri kuwa, kile unachokijua ndio usahihi wa maisha ya watu. Binadamu wote ni wanafunzi siku zote mpaka wanapoondoka Duniani.

Hekima 6
Mama yako akikuficha Baba usimlaumu. Alichokibeba anajua akikishusha kwako huwezi kustahimili.

Hekima 7.
Ukipata nafasi ya kuongea, ongea machache. Hakuna mwenye maneno mengi yakakosa hila ndani yake.

Hekima 8
Usiifanye pesa ichukue nafasi ya uwepo wako katika matukio ya kijamii. Kuna siku jamii itatuma pesa kwenye tukio lako bila uwepo wake.

Hekima 9
Usipakue chakula kingi kwa sababu ya hisia za njaa kubwa. Ni heri kuongeza kuliko kubakiza na kutupa.

Hekima 10
Kila unapopanda ngazi ya maisha waheshimu unaowaacha chini. Hao ndio watakupokea wakati unashuka.
 
Mpenda sana hekima, mwisho huwa mjima😁

methali hiyo

maana yake ukihangaika sana kutafuta hekima/ukiwa motivesheno spika, mwishowe unakuwa mjuaji mjuaji tu

sehemu kubwa ya hekima inatokana na uzoefu sio kapsheni za mitandao
 
Hekima 11
Mwanamke akikuomba afu tatu mpe afu 10 ili aongezee matumizi yake mengine 😜

Manyanza hi πŸ‘‹
 
Mpenda sana hekima, mwisho huwa mjima😁

methali hiyo

maana yake ukihangaika sana kutafuta hekima/ukiwa motivesheno spika, mwishowe unakuwa mjuaji mjuaji tu

sehemu kubwa ya hekima inatokana na uzoefu sio kapsheni za mitandao
Kijana hakuna hata moja inayokuhusu hapo hebu punguza misimamo ya kikomunisti aisee 🀣
 
Kwender 🀣🀣🀣
Tunaomba mpk mkate moto, kwanza msipoombwa hamtoi
Kuna Kibaka mmoja hapa Mtaani alistaafu ukibaka akawa anaomba omba tu watu wanamkataa. Akaanzisha kamsemo Wakiombwa hawatoi halafu na Wewe unakuja na Msipoombwa hamtoi 🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…