Heche: Watu hawana maji Dar miaka 64 baada ya uhuru, Taifa la tatu kuwa na vyanzo vingi vya maji

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
" Watu hawana maji Dar miaka 64 baada ya uhuru, Taifa la tatu kuwa na vyanzo vingi vya maji ni vizuri tukawaambia hawa watu kuwa watanzania si wajinga watanzania wanajua nyie ndio mmeingiza taifa kwenye matatizo haya kwa kuteka watu na kuiba rasilimali za nchi, kuiba uchaguzi na kuumiza watu" Makamu mwenyekiti CHADEMA Mhe. Heche John
Your browser is not able to display this video.
 
Aibu kubwa sana hii kwa utawala kandamizi wa ccm.
 
Ila maji yanatesa sana,yanakaribia kufilisi visenti kidogo mtu anavyovipata kwenye kuangaika,

Kuna wimbi la wananchi kuchimba visima sasa mitaani,washagundua wakiwasikiliza wanasiasa kiu za maji zitawaua
 
Mtu mmoja amesema juzi," Mkoa wa Mara msitugombanishe na Serikali. Hapa maji yapo "
Lakini mimi nipo Butiama kijijini,naona shida ya maji hapa.
Inashangaza.
Mimi nina tank la maji ya mvua,linatema maji mvua ikinyesha.
Lakini haiwezekani kuunganisha bomba kuwapelekea wenyewe shida ya maji.
 
heche ni muongo,
maji yanapatikana maeneo yote jiji la dar es salaam
 
Aweso ana zaidi ya miaka minne wizarani ila jana ndiyo anasema watamaliza tatizo la uhaba wa maji dar Oct 2026...Hawa majamaa ni wasanii sana ,miaka yote alikuwa wapi?

Kuna nchi wakisema wanashida ya maji wanaeleweka ila si kwa TZ.
 
Amani ni tunu yetu basi tuilinde kwa wivu mkubwa sana

don't play someone's game
 
Tuzingatie amani
amani tuilinde kwa gharama yoyote ile

Kama unataka kuoga au kuchota maji nenda baharini mtoni au ziwani
Ukishndwa sana tumia mchanga_kiazi Aweso
 
NCHI NYINGI DUNIANI WATU HUWA WANAJIONGEZA NA SI KUTEGEMEA SERIKALI. WATU TUJIFUNZE KUANDAA VYANZO VYETU KAMA VISIMA NA KUHIFADHI
 
heche ni muongo,
maji yanapatikana maeneo yote jiji la dar es salaam
Wewe jamaa, usiwe hivyo aisee.Kuna muda hizo akili zenu zinazowaza siasa na ushabiki muda wote mziweke pembeni.Watu wanavyoteseka hivi na maji kweli, unaleta ushabiki??
 
Wewe jamaa, usiwe hivyo aisee.Kuna muda hizo akili zenu zinazowaza siasa na ushabiki muda wote mziweke pembeni.Watu wanavyoteseka hivi na maji kweli, unaleta ushabiki??
kila kona ya jiji la dar es salaam maji yanatoka kwa wakati muafaka ulioelekezwa kwenye ratiba iliyotolewa na mamlaka ya maji jijini Dar es Salaam,
Na maji yanatoka vizuri tu maeneo yote kulingana na ratiba.

Heche anafaa kujitenga na uongo na kuropoka mambo ambayo hayana ukweli wowote.
Yeye yupo kwenye media mjini kueleza uongo, wakati huo kwenye eneo analoishi maji ndio yanatoka sasa kulinga na ratiba.

Zingatieni ratiba na muache porojo na uzushi
 
Mbona anachanganya mambo,hapohapo maji hapohapo 29/10, kuiba rasilimali,yuko sawa kweli!?
Kama anahofia matokeo ya zile kauli zao tutakinukisha pasikalike, tutazuwia uchaguzi by any means,atulie,dozi itamfikia tu
 
Hapo kaoga,kachamba maji ya Bomba na bado analia maji
 
Mbona anachanganya mambo,hapohapo maji hapohapo 29/10, kuiba rasilimali,yuko sawa kweli!?
Kama anahofia matokeo ya zile kauli zao tutakinukisha pasikalike, tutazuwia uchaguzi by any means,atulie,dozi itamfikia tu
huenda kachanganyikiwa kwasababu hata ukimtazama tu kuna kitu hakiko sawa ndania yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…