Heche: Tundu Lissu ni tunu ya taifa aachiwe bila masharti

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @chadematzofficial Bara John Heche @hechejohn amesema Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu ni tunu ya taifa huku akishinikiza kuachiwa kwa kiongozi huyo bila masharti.

Heche ameyasema hayo leo Januari 3, 2026 katika hotuba yake kwa taifa akimtaja Lissu kama mtu anayesimamia haki na mtetezi wa watu ambaye msimamo wake unakubalika na wengi.

"CHADEMA na watanzania tunajivunia kuwa na Tundu Lissu kama tunu ya taifa, mtetezi wa haki. Kwa sauti kubwa tunataka Tundu Lissu aachiwe bila masharti yoyote".
Your browser is not able to display this video.
 
Kawaite wazungu waje kutawala tanzania kwa mpito halafu amtoe huyo tunu ya chadomo
TAKATAKA HII
 
Mali/kitu chochote chenye thamani kubwa ambacho kimeporwa na majambazi ili kukitoa mikononi mwa hayo majambazi ni lazima kuyaonyesha majambazi hayo kuwa mali/kitu hicho wanachokishikilia hakitakuwa na thamani kwao kwa kuendelea kukishikilia kwa nguvu; badala yake ndiyo itakayokuwa njia yao ya kuangukia pua haraka sana.

WaTanzania ni muhimu sasa waelewe thamani kubwa aliyonayo Tundu Lissu kwa taifa hili.
Tundu Lissu akitaka kuondoka gerezani kwake ni rahisi sana wakati huu.
Atakubali tu kuwa hatashiriki tena kuwasumbua hao majambazi; au hata kwamba atashiriki kuwashawishi waTanzania wakubali kutawaliwa tu na majambazi.

Akitaka kufanya hivyo, leo hii hii anatoka gerezani

Yupo gerezani kwa sababu hataki kuwaweka waTanzania wenzake katika gereza la kudumu chini ya waovu hawa..
 
..kwanini anasema bara badala TANGANYIKA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…