Potelo unazikumbuka? Baada ya Kokakola kupotea!
Na yule chizi mmoja aliyejenga kibanda cha makuti pale jangwani peke yake unamkumbuka?
Baadaye nikipita pale jangwani nimekuwa nasema kimoyomoyo machizi wamekuwa wengi sana siku hizi!
Jumapili kuendesha gari mwisho saa saba mchana, zaidi ya hapo lazma uwe na kibali. TV ilikuwa TV ya znz peke yake ina ilikuwa inaonekana chenga chenga.movie ni drive in wale tuliokuwa tunakaa nje ya ukuta, ilikuwa inaitwa tiket mmbu..barabara ya migombani, basi la kamata lilikuwa linapita mpaka kule mwisho linageuza, palikuwa na bar inaitwa zena garden. Kuna siku asubuhi wanafunzi wa forozani walimtukana dereva wa basi la kamata, dereva akaamua kulipindua, mtoto wa wa mzee kiluvya akafa palepale....
sie wa kusini tulikuwa na mabasi yetu maarufu TITICO na MALOLOTA, kuna wakati basi la MALOLOTA lilipotea na abiria wote kijiji cha MANDAWA RUANGWA, likaja kuonekana baadaye.
Kusafisha tiketi ya basi kwa mafuta ya break ili kudai pesa zaidi ya kiwango halisi kwa zile sehemu ambazo warranty au garimoshi haifiki
Nakumbuka buluga! Ule mchele Kama ngano kutoka USA pamoja na maziwa ya unga ya njano kabisa zaidi ya nido hii ni kwa waliokulia vijijini
Aaah! hiyo ya kufuta ticket kwa mafuta ya break ili kuandika upya kiwango cha pesa umenikumbusha mbali sana!Ni kweli tulikuwa tunafanya hivyo,pia unatafuta na ticket nyingine inayoonyesha unatoka mji wa mbele zaidi ya ule unaotoka!.