Nimekaa chini Mtu mzima nikafikiria...
Warembo wengi sana kwenye hii Dunia...
Demu namba Nane kichwani akanijia...
Toka Moyoni sina budi kumsifia...
Mwenye Sura matata, Macho yanayoita...
Hana utata huyu Binti wa KiAfrika...
Hata mcheki alipopita anabebeka kama GITA...
Akitembea bado anatingisha...
Anapendeza Kimavazi, hata akiweka Pozi...
Mtoto anaweza akakujia hadi kwenye Njozi...
Sijui niseme akae, au niseme asimame...
Demu umbo namba NANE watu wote mumuone...