Haya ndo mambo yanayosababisha ugumu wa maisha mtaani

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
YANAYOSABABISHA HALI NGUMU MITAANI NI HAYA.

Waraka wa BASHIR YAKUB +255784482959.

1. Kuziba kwa mianya ya wizi bandarini. Kama tunasema bandari pekee ikitumika vizur inaweza kuilisha Tanzania nzima halafu hapohapo ikawa mapato yake ya zaidi ya 70% yanaingia mifukoni mwa watu, unategemea nini tena hiyo ya 70% ikizuiwa kuingia mifukoni mwa hao watu. Ni bila shaka athari zake zitaonekana maishani mwetu.

Hawa watu waliokuwa wanachezea hii 70% ambalo ni pato kubwa kabisa wana makampuni, wameajiri maelfu ya watu , wana familia,ndugu na marafiki ambao wamekuwa wakiogelea kwenye hii 70% nk, nk. Hawa maelfu walioajiriwa nao wanazo familia, wanazo biashara ndogo ambazo nazo wameajiri watu. Cheni ni ndefu kuliko niliyotaja na kwa ufupi unakuta imemgusa kila raia. Sasa hali ya uchumi inabakije vilevile baada ya hii 70% kuminywa. Katu haiwezekani lazima tuhisi(feel) maumivu.

Isipokuwa swali litakuwa Kama pesa hiyo imetoka mikononi mwa wachache na kuwa mali ya taifa kwann serikali isiirudishe mitaani ikaonekana tena kwa njia halali. Jibu litakuwa ni kwamba matokeo ya serikali kuingiza hela mtaani hayawezi kuonekana haraka. Yanaonekana baadae kupitia manufaa ya miradi.

Hela ya ubadhirifu bandarini ilikuwa ni hela nyingi mno kuwa kwenye mzunguko na kuondoka kwake ghafla hakuwezi kutuacha salama. Huu ni ukweli na lazima tuukubali.

2. Pesa ya wauza unga. Mzunguko wa hela ya unga mtaani unakadiriwa kufikia hadi tirioni 2 kwa mwaka. Pesa hii inaondokaje ghafla mtaani halafu tukabaki vilevile. Haiwezekani lazima tuhisi kupungukiwa na kitu.
Sehemu unakoziba mzunguko wa tirioni 2 katu hapawezi kubaki Kama awali. Ni patakuwa na mabadiliko tu.

3. Pesa iliyotokana na matumizi mabaya katika taasisi za serikali na ufisadi. Pesa ya rushwa, posho za hovyo, matumizi yasiyo na tija hakuna tena. Mzunguko wa pesa hii sio wa kubeza. Ulikuwa mkubwa na ulisisimua mitaani. Mameneja, wakurugenxi na viongozi wengine wa serikali walikuwa hawaulizi mara mbili katika kununua majumba ya bilioni 2 na zaidi, kujenga mahoteli, mabar na viwanja vingine vya starehe kwa pesa ambayo haitokani na mshahara.

Walikuwa hawaulizi mara mbili kuhonga magari ya milioni 30, 20 nk. Walikuwa hawaulizi Mara mbili kutoa mamilioni ya mitaji ya kuanzisha biashara kwa familia zao na wapendwa wao. Yote hii ni pesa kwenye mzunguko.

Ilikuwa ni kawaida kwa taasisi ya serikali kushikilia hata kumbi nne katika hoteli tofauti tofauti kwa kipindi cha miezi hata minne huku wakizilipia kila siku. Wamefanya mikutano au hawakufanya wanalipia tu.

Ndio maana hoteli nyingi zimefunga kumbi na waajiriwa katika kumbi hizo wamepunguzwa. Hii yote ilikuwa ni hela kwenye mzunguko. Unategemeaje kukatwa kwake ghafla kutuache kama tulivyokuwa awali. Haiwezekani jamani.

JAMBO MOJA KUBWA: Ni kwamba karibia 60% ya pesa iliyokuwa inasisimua na kuchamgamsha mitaa yetu ilikuwa ni pesa haramu/chafu. Kuondoka kwake ghafla hakuwezi kutuacha vilevile kama tulivyokuwa. Ilikuwa ni lazima tuone na kuhisi unyonge katika vipato vyetu baada ya kuondoka pesa hii.

Ila kitu kimoja ni kuwa uchumi una mazoea. Kama tulivyokuwa tumezoea kuishi kwa pesa haramu siku zinakuja ambapo tutazoea kuishi kwa pesa ambayo vyanzo vyake ni halali na hapo tutaacha kulalamika.

Lakini pia siku zinakuja ambapo manufaa makubwa ya kurudisha pesa hii mikononi mwa umma yataonekana na kila mmoja atafaidi tofauti na pesa haramu ambayo wachache ndio hufaidi.

Kwa haraka hatua zinazochukuliwa ni muhimu mno kuliko tunacholalamikia sasa.
 
Sina hata haja ya kukupigia simu ila sikubaliani kuwa hizo ndio sababu. Nasema ivi kwa sababu nimevuta kumbukumbu kuanzia kwa Mwl hali ya kifedha ilikuwa mbaya mbaya mbaya sana, alivyokuja Mzee Mwinyi watu wakapumua mambo yakawa safi kabisa, baadae akaja Ben mambo yakawa mabaya tena kilio nchi nzima watu wakawa wanashindia mlo mmoja, alivyokuja JK mirija ikafunguka watu wakawa na pesa, sasa awamu hii tena yametokea yaleyale ya kwa akina Ukapa.

Jiulize kwanini wale watatu they have something common kwenye masuala ya Uchumi na hawa wengine wawili wanaufanano?

Ukishatafakari na kuelewa point yangu basi huto tu sababu ulitwoandika tutakosa mashiko.
 
itachukua miaka 90 kwa iyo pesa kuonekana kwenye mzunguko, sio leo wala kesho

kifupi bwana mkubwa kafeli kila kitu
 
Hii nchi hata angeongoza nani,, watanzania tumezoea kulalamika bila kujituma
 
nilitarajia hela za wapiga dili zingeingia kwenye kapu la serikali,sasa mbona hata hiyo serikali haina hela,bado utafiti wako haujakamilika1
 
Sina hata haja ya kukupigia simu ila sikubaliani kuwa hizo ndio sababu. Nasema ivi kwa sababu nimevuta kumbukumbu kuanzia kwa Mwl hali ya kifedha ilikuwa mbaya mbaya mbaya sana, alivyokuja Mzee Mwinyi watu wakapumua mambo yakawa safi kabisa, baadae akaja Ben mambo yakawa mabaya tena kilio nchi nzima watu wakawa wanashindia mlo mmoja, alivyokuja JK mirija ikafunguka watu wakawa na pesa, sasa awamu hii tena yametokea yaleyale ya kwa akina Ukapa.

Jiulize kwanini wale watatu they have something common kwenye masuala ya Uchumi na hawa wengine wawili wanaufanano?

Ukishatafakari na kuelewa point yangu basi huto tu sababu ulitwoandika tutakosa mashiko.
Its like you trying to let us believe that a person's way of looking makes it all
 
Mbona hata serikali yenyewe imepigika watumishi wanaidai serikali hadi huruma
 
Waliozoea kupt pesa kirahs laxm ss walie na kusaga meno lkn cc ambao ht hcho kpnd mnachokita cha jk pesa km maji wengne tulitesek hvyohvyoo kwahyo ni sawa kbsa , kpnd ch jk nlkuwa nakul nym mara 8 kwa meez ns fmilia yng navsa ns maosha yanaenda kw kpto chng klekle na leo hkuna klchopungua kwang nashangaa kelee nyng mlizoea kula visivyohalalz, ht ck ya mwsho itakuwa hvyohvyo, kutesa kwa zamu hkuna wakuteseka milele malippo n hphp dunian. Mlifurah cna zlpokuwa xnawatembelea pesa xa bila jssho mkome cheezeen na leo mlifkr mungu ni wenu pekee yenu haaaaaa mungu ni wetu sote anaskiliza klio cha kl mmoja. Asante RAIS MAGUFULI KAZA ZAID YA HPO BABA
 
Watumishi kuidai serkl co den aliloanzisha maguful amelkuta tok kwa hao mliosema kpnd chao pesa zlkuwa nyng mbona km unakumbukumbu kpnd ch jk ambcho mnasema maisha ylkuwa mazur madereva, dr,walimu, reli, wanafunz waligoma je walogomea nn wkt pesa xlkuwa nyng c wangepewa pesa zao au wangetekelezewa madai yao hkuna kt kulikuwa na matabk makubwa cna serkln ss ni zamu ya kuish kwa mshahara km mtumish yyte co mwngne juu mwngne chn hueez acha kz watu wanatfta ht kwa salary ya lk moja
 
Yani mtu hata cash flow ya serikali inavyokuwa hajui
Kutokana topic aliyotoa ndg yetu... Kwamba ile mianya yote inayoleta pesa chafu imezibwa... Na amedai pesa... Itaaenda miradi ya uma kwa manufaa ya raia wote... LAkini hii kwa mtazamo wangu mimi watakafaidika kwa haraka ni watanzania wa sector rasmi(waajiriwa na serikali) ambao ni wachache..... Je ndg... Serikali inatakiwa ifanye nini sasa... Ili money flow iwe kama kawaida kwa watu wote kwa kupitia njia halali.... Ili private sector ambayo ndio ina watu wengi... Ifaidike... (yaani... Wakulima.. Wafanyabiashara... Wajasiriamali wote... Nk)
##Naombeni Jibu serious... Nini kifanyike????
 
Viwanda virudishwe mkuu... Mimi umri wangu mdogo ila mzee ananisimulia long time serikali ilikua na viwanda kibao so ikawa ina solve ishu za ajira, ishu ka kusindika,
Pia viwanda vitasaidia nchi kupunguza importation na hivo shillingi kupata nguvu dhidi ya dola...

Mafuta yanapanda bei shilling inashuka kwann mahindi unayokula dar yaayotoka mkoan yasipande.....
 
Back
Top Bottom