Haya ndio maneno zamani ukiyasema we ndio mjanja!

flintsky

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
654
744
wanajukwaa chit chat

kuna maneno enzi fulani ukiongea au ukiyaunganisha katika misemo inaleta ladha unaonekana mjanja wa town sana.

hebu leo tujikumbushie kwa uchache vibwagizo hivyo.japokuwa kuna maneno baadhi kipindi hicho yalikuwa na kiki kuliko sasa japokuwa yanatumika ila sio kivile!

kama "kasheshe" hili neno lilitumika sana kama ulikuwa huliongei kitambo hicho basi we ndezi kiwango cha maji ya mtera!

"mshkaji"hili neno enzi hizo lilikuwa hot sana kila mtu alitaka kulinena aonekane amelisema na anaenda na wakati huo.ilifikia mtu atasema hata kuku washkaji zangu basi aseme mshkaji tu*

"chelea pina"hii kuitikia salamu

' fuba' hii iliwakilisha pesa.

na mengine mengi mtajazia wana chit chat nisiwajazie
 
Back
Top Bottom