runyaga
JF-Expert Member
- Dec 23, 2013
- 523
- 241
- Juzi tarehe 13 Julai 2016, Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika kikao chake imetoa ufafanuzi juu ya mgogoro unaoendelea katika club ya Stand United kama ifuatavyo:-
- Kwanza, kamati imepitia vielelezo vyote na kujadiliana na wadau wa Stand United na kubaini bayana kwamba Stand United Football Club, ndiyo jina sahihi na halali lililosajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo na sio kampuni kama wanavyodai akina Amani.
- Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni na kupata uongozi mpya kwenye Klabu ya Stand United una sifa zote za kuitwa uchaguzi huru na wa haki kwa vile mchakato ulihusisha wanachama halali klabu hiyo.
- Wanachama wote wa Stand United ambao hawakushiriki uchaguzi ikiwa ni pamoja na wale waliokwenda kundi la kampuni wana uhalali wa kuendelea kuwa wanachama na kushiriki shughuli zote za Stand United kama wanachama wengine wote.
- Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa Stand United FC ni halali na ni ruksa kwao kuendesha ofisi na shughuli za Stand United kwa ujumla.
- TFF inatambua daftari la Wanachama wa Stand United lililoboreshwa kwa maelekezo yaliyotolewa kwa viongozi wa Stand United.