Hawa waztu Wapo wapi? Hatupaswi kuwasahau HATA KIDOGO. ni hazina ya Taifa

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
Nimekuwa nikiwakumbuka watu wa zamani sana katika burudani na sanaa ua uchoraji . nakumbuka namna mabvyo tulikuwa tunapata burudani na elimu kupitia michoro yao kwenye magazeti na magazne mbali mbali.Christian Gregory na Katuni yake maarufu sana miaka hiyo ya 70 na 80 ikiitwa Chakubanga, Phillip Ndunguru, Sammi Mwamkinga, Nathan Mpangala na katuni yake ya kijasti,James Gayo, Robert Mwampembwa, Francis Bonda, Oscar Makoye, Fadhili Mohamed,Marco Tibasimah, Ibra Radi Washokera n.k nakumbuka magzeti pendwa ya miaka ile kama SANI, KINGO, MSANII, na mengine kidogo yamenitoka naomba wadau turudishane miaka hiyo tukikumbuka visa mbali mbali vya akina komredi kipepe,madenge, mtaakam wa kusakata kabumbu CHONKA n,k .

Pia ningependa sana kukumbushwa anani akilikuwa mchoraji wa kitabu cha PANGALASHABA .... nakumbuka hadithi za akina Akajase Mbamba sijui ntapata wapi vitabu vile tena na magzeti hayo nliyotaja na mengineyo. tumetoka mbali sana ila hatujui tuendako.
 
Back
Top Bottom