Mimi nimefanya usahili wa mchujo uliosimamiwa na Sekretarieti pale Mwalimu Nyerere Kigamboni kwa nafasi ya Legal Officer II ofisi ya Taifa ya Uhasibu (National Audit Office).
Katika tangazo la kutuita kwenye usahili tuliambiwa usahili wa pili utafanyika tarehe 16 Desemba 2014 pale ofisi za Sekretarieti. Wao wakaweka matokea ya mchujo usiku wa tarehe 14 Desemba 2014.
Matokeo hayo yakiambatana na tangazo kwamba wale wote ambao wanatakiwa kuendelea na usahili kwa nafasi ya National Audit Office wanatakiwa kwenda kufanya usahili wa Practical Tanzania Institute of Accountancy Kurasini tarehe 15/12/2014 saa moja asubuhi.
Mimi nimeamka mapema na kuelekea ofisini kwangu saa moja ndo naona tangazo hilo, siko na vyeti wala nini. Ikabidi niwapigie watu wa Sekretarieti, wao wakanijibu kwamba matokeo yamewekwa Jumapili jioni na tangazo hilo. Nikawauliza kama kuna mabadiliko ya ghafla namna hiyo kwanini msiwapigie watu simu?
Wao wakanijibu kwamba matokeo yaliwekwa mapema jioni so nilipaswa kuyaona.Mimi nimekosa nafasi hiyo ya kushindana na wenzangu kwa haki ktk mchakato wa ajira. Ila naona sikutendewa haki kwakuwa taarifa ya usahili huu haikuwa kwangu kwa muda sahihi.
Mimi sina kitu cha kunisaidia kucheki internet nikiwa nyumbani hadi nifike ofisini saa moja asubuhi.Nadhani kama wahusika wangekuwa wanajali ningepigiwa simu kuambiwa jambo hili kwakuwa lilikuwa la ghafla sana. Lakini najiuliza mtu aliyemaliza usahili akarudi kwao Morogoro hata kama amepata taarifa hii saa moja asubuhi angeweza kuwahi usahili huu?, sidhani.
Sidhani kama Sekretarieti haina pesa ya kununua vocha kuwafahamisha wasahiliwa wasiozidi 100 waliowaita kwenye usahili.Uko wapi ufanisi wanaotambia Sekretarieti ya Ajira?.Au ndo wanaanza kufanya hujuma.