Hawa ni baadhi ya wanyama wetu walioko uarabuni miaka 10 iliyopita

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,800
34,189
Je unadhani Baadhi ya viongozi wa serikali hawahusiki usafirishaji wa wanyama pori nje ya nchi?

Twiga.jpg


 
kuna wale wanyama wanakula unga na kusafirisha na wao wako huko huko wameshikiliwa uarabuni+china+indonesia+etc.
Hapa sipo mahali pa Wanyama wanaokula unga. Hapa ni mahali pa wanyama wa porini wanao kula majani. Mkuu umekosea kabisa kujibu swali langu.
 
kuna wale wanyama wanakula unga na kusafirisha na wao wako huko huko wameshikiliwa uarabuni+china+indonesia+etc.
Kweli mkuu na kwa lugha nyepesi tunawaita punda wala punda!
Vigogo waloshikiria sekta nyeti katika inji hii ndo "matagiri" wao wanaowasafirisha!
 
Sasa mkuu MziziMkavu swali lako kuna haja ya kulijibu kweli wakati unajua fika Tanganyika yetu kuna watu wameigeuza kuwa shamba la bibi?
Hujamuona Maghembe juzi kati kaishia kumtemesha mhaya wa watu unga kisa kadili kadogo tu ka kusafirisha vijingedere!?
 
Bange ni mmea mbaya sana:eek::eek:
Ona unavyokufanya!!
Acha kusingizia bangi mkuu...alichosema Jamaa ni kweli tupu....kwani we hujui kuwa kuna wanyama walao unga wanaishi jela za Asia wamehamishwa kutoka Tanganyika?
 
Uzi km huu vijana wa Jecha huwezi kuwaona hapa.wao wanatafuta nyuzi za kujitoa ufahamu ili jioni wakapate buku saba yao Lumumba
 
kuna Lapumba National park ipo Peter'sburg South Africa Twiga wetu wapo wengi sana pale..
Hivi Twiga wanapatikana Tanzania tuu? Yaani ukimuona Twiga nje ya Tanzania ina maana ametoka Tanzania tuu? Hakuna nchi zingine zenye hawa Wanyama? Twiga wa Tanzania wana alama gani inayomfanya mtu kusema kawaona Twiga wa Tanzania nchi fulani? Naomba kueleweshwa..
 
Hivi Twiga wanapatikana Tanzania tuu? Yaani ukimuona Twiga nje ya Tanzania ina maana ametoka Tanzania tuu? Hakuna nchi zingine zenye hawa Wanyama? Twiga wa Tanzania wana alama gani inayomfanya mtu kusema kawaona Twiga wa Tanzania nchi fulani? Naomba kueleweshwa..
Katika nchi za Afrika Tanzania ndio inayo ongoza kwa kuuza Wanyama wake kiholela kwa sababu ya Viongozi fulani ndani ya Serikali wana uchu ya kuwa matajiri kwa kuuza Rasilimali zetu za asili. Ndio maan kila tukiona nje Wanyama tunadhania ndio hao hao wanyama wetu waliouzwa miak 10 iliyopita. Tuna uchungu wanyama wetu wanazidi kwisha mbugani sijuwi wakiisha hao wanyama Watalii watakuja kuona kitu gani katika mbuga za wanyama? Jiulize wewe kisha upate jibu lako.
 
Acha kusingizia bangi mkuu...alichosema Jamaa ni kweli tupu....kwani we hujui kuwa kuna wanyama walao unga wanaishi jela za Asia wamehamishwa kutoka Tanganyika?

Nasema bange kwasababu wewe na mwenzako kwanza mnashindwa kutofautisha BINADAMU na WANYAMA, hao walio kwenye magereza huko asia na kwingineko, kiustaarabu na kiungwana tunawaita binadamu (watu) na si wanyama kama mlivyoiweka nyie, haya yanawezekana yakawa ni madhara ya bange!!

Pili, mmeshindwa kuelewa kuwa hii mada haikupostiwa ili kujadili kuhusu hao wanaobeba madawa!! Simply mmebaka mada, mada inataka kitu kingine nyie mnaibuka na kitu kingine. Haya nayo ni madhara ya bange
 
Katika nchi za Afrika Tanzania ndio inayo ongoza kwa kuuza Wanyama wake kiholela kwa sababu ya Viongozi fulani ndani ya Serikali wana uchu ya kuwa matajiri kwa kuuza Rasilimali zetu za asili. Ndio maana kila tukiona nje wanyama "Tunadhania" ndio hao hao wanyama wetu waliouzwa miak 10 iliyopita Tuna uchungu wanyama wetu wanazidi kwisha mbugani sijuwi wakiisha hao wanyama Watalii watakuja kuona kitu gani katika mbuga za wanyama? Jiulize wewe kisha upate jibu lako.
Asante kwa majibu mkuu,kumbe huwa ni "Kudhani" tu?! Nilifikiri ni uhakika kua kila Twiga aliyepo uarabuni katoka Tz,ila katika maisha kuishi kwa kufuata "Dhana" huwa sio vizuri
 
Cleverking wanyama wana asili ya eneo husika iyo mbuga ni ya mtu binafsi na wengi ya wanyama wa pale wametoka maeneo tofauti kwa miaka ya nyuma hii wamejazwa sana Twiga na wengi wametoka Tanzania.South Africa ki asilia hawana Twiga hata katika mbuga zao ukiwaona ujue wamezolewa kwetu...
 
Back
Top Bottom