Dhahabu yetu inapotea bure,haisaidii uchumi wala kustabilize shilingi yetu!
Ukiifuatilia hii nchi unaweza kujinyonga kwa maudhi. Kumbe kuna makampuni kibao yanayofanya kazi ya kutuibia tu hapa nchini na si vinginevyo! Hata hao wanaokusanya kodi ni vichwa vya wendawazimu kwani hawazishtukii kampuni kama Vodacom ambayo kwa vigezo vyovyote ndiyo wanaoongoza kwa uwingi wa wateja na bei ya bidhaa zao, Tigo ambayo hivi karibuni imesomba wateja wengi kwelikweli na ambayo bidhaa zake zinatozwa sawa kabisa na Zain na hata Vodacom?Wakuu,Salaam!
Kwa wale mliofuatilia Hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa kuahirisha Bunge Jana alitoa pongezi na kuzitaja Makampuni au Mashirika yanayoongoza kwa kulipa Kodi hapa nchini.
Alisema kwa kipindi Cha mwaka 2005 na 2011 Makampuni hayo yamekuwa yakifanya vizuri katika ulipaji Kodi.
Aliyataja Makampuni hayo Kama ifuatavyo;
1. Tanzania Breweries Company(TBL) Shilingi Bilioni 165.4
2. National Microfinace Bank(NMB). Shilingi Bilioni 108.6
3. Tanzania Cigarette Company(TCC). Shilingi Bilioni 92. 1
4. National Bank of Commerce(NBC). Shilingi Bilioni 89.9
5. CRDB LTD Shilingi Bilioni 79.2
6. Tanzania Ports Authority(TPA) - Shilingi Bilioni 76.8
7. Tanzania Potland Cement - Shilingi Bilioni 73.4
8. Airtel(T) LTD - Shilingi Bilioni 63.6
9. Tanga Cement Company - Shilingi Bilioni 43.6
10. Standard Charted Bank - Shilingi Bilioni 40.0
11. City Bank. Shilingi Bilioni 35.7
12. Resolute(T) LTD. Shilingi Bilioni 32.1
13. TICTS. Shilingi Bilioni 25.9
14. Tanzania Distillers LTD. Shilingi Bilioni 13.4
15. Group Five International. Shilingi Bilioni 9.5
Haya Wakuu na tujadili na kutoa maoni yetu...
Dhahabu yetu inapotea bure,haisaidii uchumi wala kustabilize shilingi yetu!
Where's Vodacom, Geita Gold, Bulyanhulu, Artumas, Songas,North Mara, Buzwagi????????
hawalipi kodi, bado wanajiendesha kwa hasara
Kwa kila Jumanne na Alhamisi tofali za dhahabu zenye ukubwa wa tofali la kuchoma na uzito wa gramu 12000 zipatazo 400 husafirishwa kwenda nje ya nchi, Hebu jiulize Gramu 1 ya dhahabu huuzwa Tsh 65,000. Je ni kiasi gani cha fedha kinakwenda nje na je kinaweza kukidhi bajeti yetu? Pigeni hesabu kisha mnijulishe...! Je hii pesa haiweza kutuokoa na u-ombaomba kwa wazungu?
Hiyo hesabu ni kwa GGM pekee, bado wapo NORTH MARA, KAHAMA, ULYANKULU, BIHARAMULO.
Kwa nini pamoja na ukwasi huo bado tunaishi kimaskini?
MAWAZO YAKO YANAWEZA KUTUPA DIRA TUKAEPUKA KUIBIWA
MIMI NAAMINI KAMA TUKIKUSANYA KODI KWA MADINI PEKEE, MAISHA MAZURI KWA WATZ YATAPATIKANA BILA KWERE
Misingi ya makampuni kutokulipa kodi, ipo katika sheria za kifisadi kama vile SHERIA YA MADINI 2010, na SHERIA YA UWEKEZAJI TANZANIA. UKIZISOMA UTAPATA MAJIBU YA SERIKALI LEGELEGE KUSHINDWA KUKUSANYA KODI.
SHERIA HIZO NDO CHANZO CHA MAKAMPUNI KUBADILISHA MAJINA KILA UCHWAO LEO.
UDHAIFU UNAOPATIKANA KATIKA SHERIA HIZO, NI WAWEKEZAJI KULIPA KODI BAADA YA WAO KUTANGAZA KUPATA FAIDA. NANI ATATANGAZA KUPATA FAIDA KATIKA MAZINGIRA HAYA?
HAPA KWETU WENYEJI TUNALIPA KODI KULIKO WAWEKEZAJI.
WIZI MTUPU.
bado hawaja-break even. au umesahau kama wana mikataba ya miaka 100?Where's Vodacom, Geita Gold, Bulyanhulu, Artumas, Songas,North Mara, Buzwagi????????